-
Canada yataka genge la Trump litambuliwe kuwa kundi la kigaidi
Jan 26, 2021 08:25Bunge la Canada limeitaka serikali ya nchi hiyo liliweke rasmi genge la wanamgambo waliojizatiti kwa silaha na wafuasi sugu wa aliyekuwa rais wa Marekani, Donald Trump katika orodha ya magenge ya kigaidi kama vile al-Qaeda na ISIS (Daesh).
-
Balozi wa Iran UN: Rais wa Marekani achukue hatua ya kwanza
Jan 26, 2021 04:05Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amesema Jamhuri ya Kiislamu haina mpango wowote wa kufanya mazungumzo na Rais mpya wa Marekani Joe Biden, lakini inasubiri serikali mpya ya Washington ichukue hatua ya kwanza ya kuliondolea taifa hili vikwazo na kurejea katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA.
-
Ripoti: Polisi ya Marekani imeua makumi ya Wamarekani weusi tokea 2015
Jan 26, 2021 03:55Uchunguzi mpya umefichua kuwa, makumi ya Wamarekani wenye asili ya Afrika wameuawa na polisi ya nchi hiyo tokea mwaka 2015.
-
Guterres : COVID-19 imetufunza hatuwezi kupuuza hatari, ataka chanjo igaiwe kiuadilifu
Jan 26, 2021 03:43Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, amesema kuwa maambukizi ya kirusi cha corona na kuenea ugonjwa wa COVID-19 pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa, ni changamoto mbili kuu ulizoikumbwa dunia hivi sasa.
-
Kremlin yakosoa uingiliaji kati wa Marekani katika maandamano huko Russia
Jan 24, 2021 23:33Msemaji wa ikulu ya Russia (Kremlin) ameyataja matasmhi ya uingiliaji kati ya Marekani kuhusu maandamano yaliyo kinyum cha sheria huko Russia kuwa ni uingiliaji wa masuala ya ndani ya Moscow.
-
Wamarekani wakatishwa tamaa na chanjo ya corona ya Pfizer
Jan 24, 2021 23:00Baada ya kuvunja rekodi na kuongezeka sana idadi ya maambukizi na vifo vya wagonjwa wa COVID-19 nchini Marekani licha ya chanjo iliyopigiwa propaganda kubwa ya shirika la Kimarekani la Pfizer kuanza kutumika nchini humo, idadi kubwa ya wananchi wa nchi hiyo sasa wamekatishwa tamaa na utendaji kazi wa chanjo hiyo.
-
Adam Schiff ataka kutolewa ripoti kuhusu mauaji ya Jamal Khashoggi
Jan 24, 2021 04:35Mkuu wa Kamati ya Intelijinsia katika Bunge la Wawakilishi la Marekani amemwandikia barua Mkuu Mpya wa Usalama wa Taifa wa nchi hiyo akitaka kutolewa ripoti kuhusu mauaji ya mwandishi habari mkosoaji wa utawala wa Saudi Arabia.
-
Zarif: Mlango wa fursa kwa utawala mpya wa Marekani hautabaki wazi milele
Jan 23, 2021 08:19Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amemuasa Rais mpya wa Marekani Joe Biden, ahitimishe sera za mashinikizo zilizogonga mwamba za mtangulizi wake Donald Trump na kusisitiza kuwa, "dirisha la fursa kwa timu mpya ya Ikulu ya White House halitabakia wazi milele."
-
Russia yakaribisha pendekezo la Marekani la kurefusha muda wa Mkataba wa New Start
Jan 23, 2021 01:25Serikali ya Russia imeunga mkono pendekezo la Rais Joe Biden wa Marekani la kurefusha mkataba wa kupunguza silaha za kistratijia za nyuklia maarufu kwa jina la New START kwa miaka mitano.
-
Hamas: Trump alikuwa mshirika wa hujuma za utawala wa Kizayuni dhidi ya Palestina
Jan 21, 2021 08:13Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) amesisitiza kuwa Donald Trump alikuwa mshirika wa moja kwa moja wa utawala wa Kizayuni katika kuwakandamiza wananchi wa Palestina.