Serikali ya Biden kutekeleza hujuma za kimtandao dhidi ya Russia
https://parstoday.ir/sw/news/world-i67676-serikali_ya_biden_kutekeleza_hujuma_za_kimtandao_dhidi_ya_russia
Duru moja ya habari iliyo karibu na chama tawala cha Dmocrat nchini Marekani imefichua kuwa, kuna uwezekano Washington wiki tatu za karibuni ikatekeleza silsila ya hujuma za kimtandao dhidi ya Russia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 09, 2021 01:19 UTC
  • Serikali ya Biden kutekeleza hujuma za kimtandao dhidi ya Russia

Duru moja ya habari iliyo karibu na chama tawala cha Dmocrat nchini Marekani imefichua kuwa, kuna uwezekano Washington wiki tatu za karibuni ikatekeleza silsila ya hujuma za kimtandao dhidi ya Russia.

Gazeti la New York Times limeripoti kuwa, serikali ya Rais Joe Biden wa Marekani  inajiandaa kutekeleza hujuma za kimtandao dhidi ya mitandao ya Russia katika kulipiza kisasi kwa kile ilichokitaja kuwa mashambulio makubwa yaliyofanywa na Russia dhidi ya Marekani katika wiki za mwisho za kuwepo madarakani serikali ya rais wa zamani wa nchi hiyo Donald Trump. 

Serikali ya Marekani imesema inatuma ishara kwa Russia juu ya kulipiza kisasi hujuma za kimtandao dhidi yake zilizofanywa na  kampuni ya Solar Winds. 

Katika siku za karibuni vyombo vya habari nchini  Marekani viliripoti pakubwa kuhusu taarifa ya kujipenyeka wadukuzi katika taasisi mbalimbali za serikali nchini Marekani kwa kutumia programu ya kampuni ya Solar Winds yenye makao yake jimboni Texas nchini humo.  

Kampuni ya Solar Winds yenye makao yake jimboni Texas, Marekani 

Ripoti za vyombo vya habari vya Marekani zibainisha kuwa, wadukuzi wamejipenyeza katika wizara mbalimbali na mashirika zikiwemo idara husika za usalama wa taifa wa masuala ya nyuklia za nchi hiyo.