-
Uingereza yadokeza kuwa itachukua hatua zaidi dhidi ya Israel kutokana na hali ya 'kikatili' ya Ghaza
Jul 23, 2025 02:41Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza David Lammy ameonya kuwa ikiwa usitishaji vita katika Ukanda wa Ghaza hautafikiwa hivi karibuni, zinaweza kuchukuliwa hatua zaidi dhidi ya Israel.
-
Mafaili ya siri yanayohusu mauaji ya Martin Luther King Jr yawekwa hadharani
Jul 23, 2025 00:18Serikali ya Rais wa Marekani Donald Trump imeweka hadharani maelfu ya mafaili na nyaraka za serikali zinazohusiana na mauaji ya nyota wa kupigania haki za kiraia Martin Luther King Jr. Siku ya Jumatatu, kurasa zipatazo 240,000 ziliwekwa kwenye tovuti ya Hifadhi ya Taifa, ambayo imeahidi kutoa nyaraka nyingi zaidi.
-
Ripoti: Mienendo ya Netanyahu inaitia wasiwasi White House
Jul 20, 2025 10:50Baadhi ya maafisa wakuu wa Marekani wameliambia shirika la habari la Axios kwamba, hofu inaongezeka ndani ya utawala wa Donald Trump juu ya tabia na mienendo ya Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, wakielezea mienendo hiyo kama ya kutojali, kuvuruga uthabiti, na wakati mwingine yenye ukosefu wa ukomavu.
-
Serikali ya Trump kuteketeza tani 500 za chakula, dunia ikisakamwa na njaa
Jul 18, 2025 13:40Marekani inajiandaa kuharibu karibu tani 500 za chakula cha msaada wa dharura, ikiwa ni sehemu ya hifadhi kubwa ya tani 60,000 za chakula hicho iliyokwama katika maghala katika sehemu mbalimbali duniani, huku njaa ikiongezeka kote ulimwenguni.
-
Afisa wa zamani wa Pentagon: Huenda US ikaishiwa na makombora
Jul 18, 2025 10:44Mshauri wa zamani wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon), Douglas Macgregor ameonya kuwa, Marekani inaweza kuishiwa na hifadhi yake ya makombora ndani ya siku nane.
-
Jibu la suali la leo; nini sababu ya waziri wa zamani wa mambo ya nje wa US kukosoa sera ya Trump kuhusiana na Iran?
Jul 18, 2025 08:53Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Anthony Blinken, amekosoa mwelekeo wa rais wa nchi hiyo Donald Trump kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran; na licha ya kuibua madai mengine mapya amesema: Iran bado haijaamua kuunda silaha za nyuklia na imetekeleza ahadi zake katika JCPOA.
-
Rais wa Brazil asema, Trump ni rais wa Marekani, si ‘mtawala mkuu’ wa dunia
Jul 18, 2025 03:27Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva amepinga tangazo la Rais wa Marekani Donald Trump la kuongeza ushuru wa asilimia 50 kwa bidhaa zinazoingizwa Marekani kutokana nchini humo, na kuapa kuwa "atajibu mapigo" dhidi ya hatua hiyo na kutetea maslahi ya watu wake.
-
Eswatini kuwatimua wahamiaji 'sugu' kutoka US baada ya malalamiko
Jul 17, 2025 01:29Serikali ya Eswatini ilisema jana Jumatano kwamba, inawashikilia raia watano wa nchi ya tatu waliofukuzwa kutoka Marekani katika magereza yaliyotengwa, chini ya makubaliano na utawala wa Rais Donald Trump, lakini inapania kuwarejesha katika nchi zao.
-
Nini lengo la Umoja wa Ulaya katika kuzidisha vikwazo dhidi ya Iran?
Jul 16, 2025 23:05Umoja wa Ulaya, ukifuata nyayo za Marekani, umeendeleza siasa za kuzidisha mashinikizo dhidi ya Iran katika nyanja mbalimbali katika muhula wa pili wa uongozi wa Donald Trump kwa shabaha ya kuilazimisha Tehran isalimu amri mbele ya matakwa ya kupindukia mipaka ya nchi za Magharibi.
-
US yaweka rekodi mpya ya kuogofya, yatimua maelfu ya watoto
Jul 15, 2025 01:13Zaidi ya watoto 8,300 wahamiaji wasio na vibali, wenye chini ya umri wa miaka 11 walipewa maagizo ya kufukuzwa nchini Marekani mwezi Aprili, hiyo ikiwa ni idadi ya juu zaidi ya kila mwezi kuwahi kurekodiwa nchini humo.