-
Iran: Rais Rouhani hana mpango wowote wa kukutana na Trump
Sep 16, 2019 22:45Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amepuuzilia mbali uwezekano wowote wa Rais Hassan Rouhani kukutana na Rais wa Marekani Donald Trump katika mkutano ujao wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York.
-
Sisitizo la Russia la kushirikiana na Iran kwa ajili ya kuanzisha mfumo mbadala wa SWIFT
Sep 14, 2019 22:04Vikwazo vya nchi za Magharibi dhidi ya Russia na Iran vinavyotekelezwa kwa visingizio mbalimbali vimezifanya nchi mbili hizi zifanye mashauriano lengo likiwa ni kutafuta njia za kukabiliana navyo. Russia inaitazama Iran kama nchi mshirika wake yenye maslahi ya pamoja ya pande mbili na wakati huo huo inatilia maanani suala la kuimarisha msimamo wa Iran katika kukabiliana na Magharibi hususan Marekani.
-
Njama za utawala wa Trump za kuficha namna Saudi Arabia ilivyohusika katika matukio ya Septemba 11
Sep 14, 2019 02:56Baada ya matukio ya Septemba 11 mwaka 2001, Marekani ilijinadi kama mbeba bendera ya vita dhidi ya ugaidi duniani na kwa kisingizio hicho ikatekeleza mashambulizi kadhaa ya kijeshi kukiwemo kuzivamia Iraq na Afghanistan. Pamoja na hayo, sera za Marekani katika vita dhidi ya ugaidi zimekuwa na mgongano na undumakuwili mkubwa.
-
Zarif: Marekani haihitaji adui ikiwa na rafiki kama Israel
Sep 13, 2019 23:11Huku kukiwa na ripoti kuwa utawala haramu wa Israel umeweka vifaa vya ujasusi karibu na Ikulu ya White House, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amewakejeli wakuu wa Washington na kusema, Marekani ikiwa na muitifaki ambaye anafanya ujasusi dhidi yake basi haihitaji maadui.
-
Marekani: Sera za mashinikizo ya kiwango cha juu kabisa dhidi ya Iran zitaendelea
Sep 13, 2019 03:39Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani amesema, mashinikizo ya kiwango cha juu kabisa ya nchi hiyo dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yataendelea.
-
Israel yatuhumiwa kuweka vifaa vya ujasusi karibu na White House
Sep 12, 2019 22:08Serikali ya Marekani inautuhumu utawala wa Kizayuni wa Israel kuwa umefunga vifaa vidogo vya ujasusi karibu na Ikulu ya White House na maeneo mengine muhimu mjini Washington D.C.
-
Kutambuliwa kimataifa kwamba mashambulizi ya Marekani nchini Syria ni jinai ya kivita
Sep 12, 2019 05:55Muungano wa kimataifa wa eti kupambana na Daesh (ISIS) unaoongozwa na Marekani uliundwa mwaka 2014 kwa madai ya kukabiliana na genge hilo la kigaidi, na umekuwa ukifanya mashambulizi ya kiholela nchini Syria bila ya kuwa na taathira zozote za maana mbaya kwa genge hilo la ukufurishaji.
-
UN: Mashambulizi ya Marekani nchini Syria ni sawa na jinai za kivita
Sep 12, 2019 03:24Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, mashambulizi yanayofanywa na Marekani na washirika wake huko Syria ni sawa na jinai za kivita.
-
Rouhani: Ni lazima Marekani iachane na sera zake za vita na mashinikizo
Sep 11, 2019 23:37Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, stratijia ya taifa la Iran katika kukabiliana na mashinikizo ya kiwango cha juu zaidi ni kusimama kidete. Ameongeza kuwa: "Ni lazima Marekani iweke kando sera zake za kupenda vita na mashinikizo ya kiwango cha juu kabisa."
-
Iran: Hatufanyi mazungumzo na Marekani iwapo wanaendeleza ugaidi wa kiuchumi
Sep 11, 2019 02:59Mwakilishi wa kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amesema ni jambo lisilowezekana kwa Jamhuri ya Kiislamu kufanya mazungumzo na Marekani madhali serikali ya Washington inaendeleza ugaidi wa kiuchumi na kuliwekea vikwazo taifa hili.