Israel yatuhumiwa kuweka vifaa vya ujasusi karibu na White House
https://parstoday.ir/sw/news/world-i55969-israel_yatuhumiwa_kuweka_vifaa_vya_ujasusi_karibu_na_white_house
Serikali ya Marekani inautuhumu utawala wa Kizayuni wa Israel kuwa umefunga vifaa vidogo vya ujasusi karibu na Ikulu ya White House na maeneo mengine muhimu mjini Washington D.C.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 12, 2019 22:08 UTC
  • Israel yatuhumiwa kuweka vifaa vya ujasusi karibu na White House

Serikali ya Marekani inautuhumu utawala wa Kizayuni wa Israel kuwa umefunga vifaa vidogo vya ujasusi karibu na Ikulu ya White House na maeneo mengine muhimu mjini Washington D.C.

Hayo yaliripotiwa jana Alkhamisi na shirika la habari la Politico ambalo liliwanukuu maafisa watatu wa zamani wa serikali ya Washington wenye ufahamu wa habari hizo.

Kwa mujibu wa maafisa hao, moja ya vifaa hivyo vya kijasusi ni “StingRays” yenye uwezo wa kudukua mawasiliano ya simu. Duru za habari zinasema yumkini utawala haramu wa Israel ulipachika vifaa hivyo karibu na Ikulu ya White House katika kipindi cha miaka miwili iliyopita ili ufuatilie mawasiliano ya simu ya Rais Donald Trump. 

Hii ni katika hali ambayo, Trump hajatoa kauli yoyote ya kulaani au kukosoa ujasusi huo wa Wazayuni dhidi ya utawala wake. Utawala haramu wa Israel umetoa taarifa ya kukanusha tuhuma hizo dhidi yake. 

Baadhi ya vifaa vya ujasusi vya Wazayuni

Si vibaya kukumbusha hapa kuwa, viongozi wa White House waliwahi kudai kuwa serikali ya Barack Obama ilishirikiana na Kitengo cha Mawasiliano cha Serikali ya Uingereza (GCHQ) wakati wa uchaguzi uliopita wa Rais wa Marekani na kumfanyia ujasusi Trump na timu yake ya uchaguzi.

Kitengo cha Mawasiliano cha Serikali ya Uingereza kilitoa taarifa na kukanusha kuingilia kivyovyote kwenye uchaguzi wa rais wa Marekani na kupinga tuhuma hizo.