-
Marekani yakosolewa kwa kukusudia kuangamiza mfumo wa usalama duniani
Sep 03, 2019 02:26Rais Donald Trump wa Marekani amevuruga na kuhatarisha sana usalama wa kimataifa kwa kuendeleza sera zake zenye utata za kukiuka kanuni na mikataba ya kimatafa, hasa ya kujiondoa katika mikataba ya kudhibiti silaha hatari duniani.
-
Marekani yatuma ndege za kiistratijia za kivita nchini Uingereza huku UK ikipigania kujitoa EU
Sep 02, 2019 03:11Afisa mmoja wa jeshi la anga la Marekani amesema kuwa Washington imetuma ndege zake za kiistratijia za B-2 nchini Uingereza kama njia ya kuonesha kuwa iko pamoja na serikali ya nchi hiyo.
-
Marekani yajaribu kufanya tena mazungumzo na Korea ya Kaskazini
Sep 01, 2019 23:36Viongozi wa Marekani wanajaribu kila linalowezekana kufanya tena mazungumzo na Korea ya Kaskazini kufuatia tahadhari iliyotolewa na serikali ya Pyongyang.
-
Sisitizo la Rais Erdogan wa Uturuki la kununua ndege za kivita za Russia
Sep 01, 2019 23:35Kufuatia hatua ya Uturuki ya kununua mfumo wa makombora wa S-400 kutoka Russia, wakuu wa nchi hiyo sasa wameazimia kununa ndege za kisasa za kivita za Russia za Sukhoi-35 na Sukhoi-57.
-
Iran yajibu vitisho vya Marekani: Tutauza mafuta kwa yeyote na kwa washitiri wote
Sep 01, 2019 03:23Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema Marekani inatumia "uharamia na vitisho" kuizuia Iran isiuze mafuta yake, lakini Jamhuri ya Kiislamu itaendelea kuuza mafuta yake kwa yeyote na kwa wanunuzi wote.
-
Umaarufu wa Trump wazidi kupungua kote Marekani
Aug 31, 2019 11:38Umaarufu wa Rais Donald Trump wa Marekani unazidi kupungua kwa kasi nchini humo huku uchaguzi mkuu wa 2020 ukikaribia. Kwa mujibu wa uchunguzi wa maoni uliofanyika hivi karibuni, umaarufu wa Trump umepungua miongoni mwa wanawake wa Marekani.
-
Sisitizo la Trump la kuendelea kuwepo askari wa Marekani nchini Afghanistan
Aug 31, 2019 02:08Miaka 18 iliyopita Marekani iliishambulia na kuivamia kijeshi Afghanistan na kisha ikaikalia kwa mabavu nchi hiyo kwa kisingizio cha kulipiza kisasi cha mashambulio ya Septemba 11, mwaka 2001 na pia kupambana na ugaidi nchini humo. Wakati rais wa sasa wa Marekani Donald Trump alipokuwa kwenye kampeni za uchaguzi wa urais mwaka 2016 na baada ya kuingia Ikulu ya White House aliahidi kwamba atawaondoa askari wa nchi hiyo walioko Syria na Afghanistan, hata hivyo hadi sasa amehalifu ahadi yake hiyo.
-
Hatibu wa Swala ya Ijumaa Tehran: Marekani ni kinara wa tawala za kigaidi duniani
Aug 30, 2019 07:29Hatibu wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesema kuwa, Marekani ni kinara wa tawala za kigaidi kote duniani na kwamba, baada ya maafisa wa serikali ya Washington kukiri kwamba nchi hiyo ndiyo iliyoanzisha makundi ya kigaidi katika eneo la Mashariki ya Kati, ni aibu kubwa kwa Marekani kudai kuwa inapambana na ugaidi.
-
Zarif: Lazima Marekani isitishe ugaidi wa kiuchumi na irejee JCPOA, kabla ya mazungumzo
Aug 30, 2019 03:30Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Mohammad Javad Zarif amesema Marekani lazime irejee katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA na isitishe ugaidi wake wa kiuchumi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kabla ya kufanyika mazungumzo.
-
Kudumu kwa JCPOA kunategemea hatua za kivitendo za Ulaya, si kufanya mazungumzo na Marekani
Aug 29, 2019 07:43Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayehusika na masuala ya kisiasa amesema, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haitaruhusu Marekani iyatumie vibaya kwa manufaa yake mazungumzo ya Iran na nchi za Ulaya.