Umaarufu wa Trump wazidi kupungua kote Marekani
(last modified Sat, 31 Aug 2019 16:08:39 GMT )
Aug 31, 2019 16:08 UTC
  • Donald Trump
    Donald Trump

Umaarufu wa Rais Donald Trump wa Marekani unazidi kupungua kwa kasi nchini humo huku uchaguzi mkuu wa 2020 ukikaribia. Kwa mujibu wa uchunguzi wa maoni uliofanyika hivi karibuni, umaarufu wa Trump umepungua miongoni mwa wanawake wa Marekani.

Jarida la Hill limeandika kuwa, uchunguzi wa maoni uliofanywa na Chuo Kikuu cha Quinnipiac umeonesha kuwa, Rais Donald Trump amepoteza umaarufu miongoni mwa wanawake kwa asilimia 23 ikilinganishwa na wagombea wengine watano maarufu wanaotazamiwa kuwania kiti cha urais katika uchaguzi wa mwaka 2020. Uchunguzi huo umebaini kuwa wanawake wengi wazungu ambao walimpigia kura Rais Trump mwaka 2016, hawatampikia kura mwaka 2020.

 Uchunguzi huo umebaini kuwa, makamu wa rais wa zamani wa Marekani Joe Biden wa chama upinzani za cha Democrat na mgombea huru Bernie Sanders wameonekana kufanya vyema zaidi ya Trump na kila mmoja wao ameshuhudia ongezeko la umaarufu kwa asilimia 18 miongoni mwa wanawake wazungu. Hali hiyo imemlazimisha Trump kuanzisha kampeni ya 'Wanawake wanaomuunga mkono Trump'. Hayo yanajiri katika hali ambayo hadi sasa wanawake 12 wamemtuhumu Trump kuwa amewadhalilisha kijinsia.

Umashuhuri wa Trump wazidi kuporomoka

Kwingineko uchunguzi mwingine wa maoni uliofanywa kitaifa na  Chuo Kikuu cha Quinnipac unaonyesha kuwa Joe Biden, Seneta wa Massachusetts Elizabeth Warren, Bernie Sanders, Seneta wa California Kamala Harris na Meya wa South Bend, Indiana, Pete Buttigieg wote wako mbele ya  Trump kwa asilimia kubwa katika kinyangnayiro cha urais 2020.

Biden yuko mbele zaidi kwa umashuhuri ambapo anamuongoza Trump kwa pointi 16 yaani asilimia 54 kwa 38.

Tags