Iran: US itabeba dhima ya shambulio lolote la Israel dhidi yetu
(last modified 2024-10-19T07:20:04+00:00 )
Oct 19, 2024 07:20 UTC
  • Iran: US itabeba dhima ya shambulio lolote la Israel dhidi yetu

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema Marekani inapasa kubebeshwa dhima ya shambulio lolote tarajiwa la Israel dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.

Katika ujumbe alioutuma kwenye mtandao wa kijamii mapema leo, Sayyid Abbas Araghchi ameeleza bayana kwamba, upande au mtu yeyote mwenye ufahamu wa jinsi na lini Israel itaishambulia Iran, anapaswa kuwajibishwa na kubeba dhima ya taathira hasi za shambulio hilo.

Akirejelea matamshi ya hivi karibuni ya Rais wa Marekani, Joe Biden akisema kwamba alikuwa na wazo bora la jinsi na lini Israel itaishambulia Iran, Araghchi amesisitiza kuwa, yeyote atakayeunga mkono shambulio la Israel dhidi ya Iran awe tayari kuwajibikia jinai hiyo.

Viongozi wapenda shari wa utawala haramu wa Israel wameahidi kuishambulia Iran eti kujibu Operesheni ya Kweli ya Ahadi 2 ya Jamhuri ya Kiislamu.

Oktoba Mosi, Iran ilivurumisha mamia ya makombora ya balestiki na kupiga kambi za kijasusi na kijeshi za utawala katili wa Israel, kama sehemu ya Operesheni ya Kweli ya Ahadi 2.

Operesheni hiyo ilikuja kujibu mauaji ya kigaidi ya viongozi wakuu wa kambi ya Muqawama wa Palestina na Lebanon, na kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), yaliyofanywa na Wazayuni maghasibu.

 

Tags