-
Mamia wapambana na polisi Tunisia baada ya muuza sigara kuuawa kwa buldoza
Oct 13, 2020 22:53Mamia ya waandamanaji waliokuwa wakirusha mawe walipambana na polisi katika mji wa Sbeitla nchini Tunisia jana Jumanne baada ya mamlaka kushambulia kibanda cha sigara ambacho hakina leseni, na kumuua mmiliki wake aliyekuwa amelala ndani yake.
-
Genge la wabeba silaha lafanya tena mashambulio na kuua 12 Ethiopia
Oct 13, 2020 04:10Kwa akali watu 12 wameuawa katika shambulizi la wanamgambo waliobeba silaha katika eneo la Benishangul-Gumuz, magharibi mwa Ethiopia.
-
Meya wa New York awataka mamea wenzake kususia mkutano wa "Urban 20" kupinga ukiukwaji wa haki za binadamu Saudia
Sep 27, 2020 01:11Meya wa jiji la New Yorkk nchini Marekani amesema kuwa atasusia mkutano wa "Urban 20" wa mameya wa miji mikubwa ya nchi wanachama katika kundi la G20 uliopangwa kufanyika nchini Saudia ili kupinga ukiukaji wa haki za binadamu na mauaji yaliyofanywa na utawala huo dhidi ya mwandishi habari Jamal Khashoggi.
-
Afrika Kusini yakadhibisha tuhuma za Marekani dhidi ya Iran
Sep 19, 2020 06:34Baada ya Marekani kujiondoa katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA, serikali ya Rais Donald Trump ilizidisha mashinikizo ya kiwango cha juu dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa shabaha ya eti kulemaza uchumi wa Iran na imekuwa ikitumia kila liwezekanalo kuanzisha vita vya kinafsi na kisaikolojia ikiwa ni pamoja na kutoa vitisho dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.
-
Watu 58 wauawa katika mashambulizi ya ADF mashariki mwa Kongo DR
Sep 11, 2020 02:42Watu wasiopungua 58 wameuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa katika mashambulio ya wanamgambo wa ADF wa Uganda katika mkoa wa Ituri mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
-
U.N: Maisha ya daktari wa Congo DR aliyeshinda tuzo ya Nobel, yamo hatarini
Aug 28, 2020 22:08Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa maisha ya daktari wa Congo ambaye alishinda Tuzo ya Amani ya Nobel kwa kazi yake ya kutibu waathirika wa ubakaji katika vita yamo hatarini baada ya kutolewa vitisho kadhaa vya kumuua.
-
Watu 13 wauawa katika shambulio la genge la waasi wa ADF mashariki mwa Congo
Aug 22, 2020 07:49Watu wasiopungua 13 wameuawa katika shambulio lililofanywa na waasi wa kundi la The Allied Democratic Forces (ADF) kutoka Uganda huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
-
Mamia ya wahajiri wa Kiethiopia wauawa kwa kupigwa risasi na askari wa Saudia
Aug 13, 2020 22:27Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limeripoti kuwa makumi ya wahajiri wa Kiethiopia waliokimbia vita kaskazini mwa Yemen wameuawa kwa kupigwa risasi na askari wa mpakani wa Saudi Arabia.
-
Bin Salman aitwa mahakamani Washington kujibu tuhuma za kutaka kumuua al Jabri
Aug 11, 2020 01:04Mahakama ya Washington DC imemtaka mrithi wa ufalme wa Saudi Arabia, Muhammad bin Salman na wenzake 13 kufika mahakamani kujibu tuhuma za kufanya jaribio la kutaka kumuua kigaidi Saad al Jabri, mkuu wa zamani wa Idara ya Intelijensia la Saudi Arabia aliyekimbilia nchini Canada.
-
Washington Post: Saudia inaongozwa na mwanamfalme wa makundi ya mauaji
Aug 10, 2020 05:21Gazeti la Washington Post la Marekani limefanya ulinganisho baina ya mauaji yaliyofanywa na Saudi Arabia dhidi ya mwandishi habari na mkosoaji wa utawala wa kifalme wa nchi hiyo, Jamal Khashogi, na jaribio la mauaji ya kigaidi lililofanywa na watu wa karibu na mrithi wa ufalme wa nchi hiyo Muhammad bin Salman dhidi ya mkuu wa zamani wa Idara ya Intelijensia la Saudi Arabia, Saad al Jabri na kusema Saudi Arabia inaongozwa na mrithi wa ufalme anayesimamia makundi ya mauti.