Nov 09, 2020 12:12 UTC
  • Sayyid Ibrahim Raisi
    Sayyid Ibrahim Raisi

Mkuu wa Vyombo vya Mahakama vya Iran amesisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imedhamiria kwa dhati kutekeleza kwa uadilifu kwa wale wote walioamuru na waliotekeleza jinai ya kumuuwa kigaidi Kamanda Qassem Soleimani.

Sayyid Ibrahim Raisi leo ameashiria kushindwa Donald Trump katika uchaguzi wa rais wa Marekani na kueleza kuwa: Gaidi ambaye ni muungaji mkono wa magaidi na ambaye mikono yake imejaa damu ya Kamanda Soleimani, shujaa wa mapambano dhidi ya ugaidi, ametimuliwa White House.  

Shahidi Kamanda Qassim Soleimani

Raisi ameeleza kuwa kuuliwa kigaidi Kamanda Soleimani ni suala linalofiatiwa wka nguuvu zote.  

Luteni Jenerali Qassem Soleimani aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) alielekea Iraq kufuatia mwaliko rasmi wa viongozi wa nchi hiyo aliuawa shahidi tarehe 3 Januari mwaka huu katika shambulio la anga la wanajeshi vamizi na magaidi wa Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad Iraq akiwa pamoja na Abu Mahdi al Muhandis Naibu Mkuu wa Kikosi cha Kujitolea cha Wananchi wa Iraq (Hashdu Shaabi) na wenzao wanane. Kamanda Soleimani alikuwa safarini nchini Iraq kwa mwaliko wa Waziri Mkuu wa nchi hiyo.

Tags