Umoja wa Afrika walaani mauaji ya raia nchini Nigeria
Nchi ya Nigeria inaendelea kukumbwa na hali ya machafuko baada ya askari usalama kuwatawanya kikatili vijana walioandamana dhidi ya ghasia za polisi, na kuua watu kadhaa. hayo yametangaza na shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International.
Ripoti zinasema kuwa, wakazi wengi wamelazimika kujifungia majumbani mwao huko Lagos, Jiji na jimbo lenye watu milioni 20 ambapo sheria ya kutotoka nje, iliyotangazwa Jumanne jioni, imeongezwa muda hadi saa 72.
Jana Jumatano visa vya uporaji na uharibifu mkubwa viliripotiwa katika maeneo kadhaa ya Jiji la Lagos, na barabara nyingi zilikuwa na vizuizi vilivyowekwa na makundi ya watu waliokuwa na hasira.
Rais wa Tume ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat amelaani vurugu zinazoendelea nchini Nigeria
Awali Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alitoa wito wa kukomeshwa kile alichokiita “ukatili” wa polisi nchini Nigeria, nchi ambayo imekumbwa na maandamano kwa wiki mbili sasa.
Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amesema katika taarifa kuwa Guterres amevihimiza vikosi vya usalama vya Nigeria kujiuzia na amewataka raia kufanya maandamana kwa amani na kujiepusha na machafuko.
Maandamano zaidi yameshuhudiwa kote nchini Nigeria kupinga mieiendo ya kikosi maalum cha polisi wa kukabiliana na wizi (SARS) kinacholaumiwa kwa kuendesha vitendo vya kikatili nchini humo.