Pars Today
Maelfu ya watu wamefanya maandamano katika miji mbalimbali ya Marekani wakipinga sera na siasa za kuwapiga vita wahajiri hususan hatua ya Rais wa nchi hiyo, Donald Trump ya kuwatenganisha watoto wahajiri na wazazi wao.
Mahakama ya Jimbo la Virginia nchini Marekani imeitaja marufuku mpya ya Rais Donald Trump wa nchi hiyo inayowazuia raia wa baadhi ya nchi kuingia Marekani, kuwa inawabagua Waislamu.
Shirika la kimataifa la misaada ya kibinadamu la CARE International limesema zaidi ya watu milioni 70 wamenasa katika migogoro iliyotelezwa na kupuuzwa kote duniani.
Uchunguzi wa maoni uliofanywa na mashirika ya misaada ya kibinadamu umebaini kuwa, mgogoro mkubwa wa kibinadamu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ndio uliopuuzwa zaidi katika mwaka huu unaomalizika wa 2017.
Viongozi wa nchi saba za Kiafrika na Ulaya wamekutana nchini Ufaransa kwa ajili ya kuchunguza namna ya kupunguza wimbi la uhajiri kutoka nchi za Afrika kuelekea barani Ulaya.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria amesema kuwa, mitandao ya magendo ya binaadamu inatishia usalama na amani ya nchi zote duniani.
Mfalme Mohammed VI wa Morocco imetoa mwito kuzitaka nchi za Afrika kuchukua hatua ya pamoja kwa ajili ya kukabiliana na wimbi la uhajiri.
Serikali za Uhispania, Ufaransa na Niger zimeunda muungano wa pamoja kwa ajili ya kupambana ipasavyo na kadhia ya wahajiri haramu na magendo ya binaadamu.
Raia wengi wa Sudan Kusini wamelazimika kuihama nchi hiyo na kukimbilia katika nchi jirani kutokana na mgogoro wa kisiasa na mauaji yanayoendelea nchini humo.
Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limewakosoa viongozi wa dunia kwa kushindwa kuupatia ufumbuzi mgogoro wa wakimbizi duniani.