-
Israel yaendelea kuwazuia Wapalestina kuswali Masjidul Aqsa
Feb 28, 2026 02:19Jeshi la Israel jana lilipeleka idadi kubwa ya wanajeshi katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu, hasa katika vituo vya ukaguzi vinavyoelekea katika mji wa Quds (Jerusalem), sanjari na kuimarisha vizuizi dhidi ya Wapalestina waliotaka kuingia katika Msikiti wa al-Aqsa kwa ajili ya Swala ya Ijumaa ya pili ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
-
Licha ya vizuizi vikali vya Israel, Wapalestina laki moja wasali I'sha na Tarawehe Masjidul-Aqsa
Feb 21, 2026 11:07Licha ya vizuizi vikali vilivyowekwa na utawala wa Kizayuni wa Israel vya kuingia katika Msikiti wa Al-Aqsa, makumi ya maelfu ya Wapalestina jana usiku walihudhuria katika msikiti huo mtukufu kusali Sala za I'sha na Tarawehe wakati huu wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
-
Israel yawazuia Wapalestina kuswali Ijumaa ya kwanza ya Ramadhani al-Aqsa
Feb 20, 2026 13:07Utawala wa Kizayuni wa Israel umewawekea vizuizi vikali Wapalestina kuingia katika Msikiti wa al-Aqsa katika mji wa Quds unaokaliwa kwa mabavu, kwa ajili ya Swala ya Ijumaa ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, huku mamia ya watu wakipanga foleni kwenye kizuizi cha Qalandiya karibu na Ramallah wakitarajia kuingia.
-
Alkhamisi, Agosti 21, 2025
Aug 21, 2025 02:59Leo ni Alkhamisi tarehe 27 Mfunguo Tano Safar 1447 Hijria, mwafaka na tarehe 21 Agosti 2025.
-
Mufti wa Moscow: Kuingia waziri Mzayuni katika Msikiti wa Al-Aqsa ni hatua ya kichochezi
Aug 06, 2025 03:55Naibu Mkuu wa Idara ya Masuala ya Dini ya Kiislamu ya Russia kwa ajili ya Masuala ya Kimataifa na Hija na Mufti wa Mkoa wa Moscow amesema: Waislamu wa Russia wanaitambua hatua ya Itamar Ben-Gvir ya kuvamia na kuingia katika Msikiti wa Al-Aqsa kuwa ya kichochezi.
-
Ben-Gvir awaruhusu walowezi wa Kizayuni kuimba na kudansi kwenye Msikiti wa Al-Aqsa
Jun 28, 2025 05:52Waziri maluuni wa mambo ya ndani wa utawala wa Kizayuni wa Israel Itamar Ben-Gvir ametoa ruhusa kwa walowezi haramu wa Kizayuni kuimba na kudansi kwenye eneo la Msikiti wa Al-Aqsa katika mji wa Baitul-Muqaddas unaokaliwa kwa mabavu.
-
Jordan yawashutumu walowezi wa Israel kuingia kwa nguvu Al-Aqsa
Jun 04, 2025 02:47Wizara ya Mambo ya Nje na Masuala ya Wageni ya Jordan imelaani vikali vitendo vya mara kwa mara vya walowezi wa Kizayuni kuvamia Msikiti wa Al-Aqsa.
-
Palestina: Walowezi wa Kizayuni wenye misimamo ya chuki wanachochea Msikiti wa Al-Aqsa uripuliwe
Apr 20, 2025 05:33Wizara ya Mambo ya Nje ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina imetoa indhari kutokana na kuongezeka uchochezi unaofanywa na makundi ya walowezi wa Kizayuni wa mrengo wa kulia wanaotaka kubomolewa Msikiti wa Al-Aqsa ulioko Baitul-Muqaddas Mashariki inayokaliwa kwa mabavu.
-
Walowezi 1000 wa Kizayuni wavamia Msikiti wa Al-Aqsa huku wakilindwa na wanajeshi wa Israel
Apr 16, 2025 02:21Katika siku ya tatu ya sikukuu ya pasaka ya Kiyahudi, walowezi elfu moja wa Kizayuni, huku wakisindikizwa na kupewa ulinzi na wanajeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel wamevamia eneo la Msikiti mtukufu wa Al-Aqsa katika mji wa Baitul-Muqaddas Mashariki unaokaliwa kwa mabavu.
-
Waziri mlowezi wa Kizayuni avamia tena Msikiti wa Al-Aqsa, Wapalestina wazuiwa wasiingie kusali
Apr 02, 2025 11:30Duru za habari zimeripoti kuwa, waziri wa usalama wa ndani wa utawala wa Kizayuni mwenye misimamo mikali ya chuki amevamia tena Msikiti Mtukufu wa Al-Aqsa huku akilindwa na kusindikizwa na vikosi vya usalama vya utawala huo ghasibu.