-
Kiongozi wa Myanmar atetea mauaji yanayotekelezwa dhidi ya Waslamu wa Rohingya
Sep 19, 2017 07:40Kiongozi wa Myanmar hatimaye amevunja kimya chake kuhusiana na jinai na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu unaotekelezwa na magaidi wa Kibudha pamoja na jeshi la nchi hiyo dhidi ya Waislamu wa Rohingya wanaoishi katika jimbo la Rakhine, ukiukaji ambao Umoja wa Mataifa umeutaja kuwa ni sawa na maangamizi ya kizazi dhidi ya Waislamu hao.
-
HRW: Jeshi la Myanmar liadhibiwe kwa kutekeleza maangamizi ya kimbari dhidi ya Waislamu
Sep 18, 2017 13:57Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limetaka vikwazo vikali vya kimataifa viwekewe Jeshi la Myanmar kutokana na kampeni yake ya kutekeleza maangamizi ya kimbari dhidi ya Waislamu wa jamii ya Rohingya.
-
Antonio Guterres amtaka Suu Kyi azuie mauaji ya Waislamu wa Myanmar
Sep 17, 2017 12:56Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amemkosoa vikali Aung Suu Kyi, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Myanmar na mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel na kumtaka achukue hatua za kusitisha mauaji dhidi ya Waislamu wa Rohingya.
-
Ayatullah Khatami: Mauaji dhidi ya Waislamu wa Myanmar, ni maafa makubwa ya kibinaadamu
Sep 15, 2017 13:57Khatibu wa Swala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo hapa mjini Tehran, Ayatullah Sayyid Ahmad Khatami amesema kuwa, mauaji kuwalenga Waislamu wa Myanmar ni maafa makubwa ya kibinaadamu na kwamba, utawala haramu wa Israel unahusika nyuma ya pazia katika mauaji na kuwafanya malaki ya Waislamu kuwa wakimbizi.
-
Kamisheni ya Ulaya: Utumiaji mabavu dhidi ya Waislamu wa Myanmar unasikitisha mno
Sep 15, 2017 03:49Mkuu wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya amelaani vitendo vya utumiaji mabavu dhidi ya Waislamu wa jamii ya Rohingya wa nchini Myanmar na kuvitaja kuwa ni maafa ya kusikitisha mno.
-
Jumuiya ya Waislamu wa Suni Pakistan: Iran ndio muungaji mkono wa kweli kwa Waislamu wa Myanmar
Sep 14, 2017 04:37Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu wa Suni nchini Pakistan amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni muungaji mkono wa kweli kwa Waislamu wa Rohingya wanaokandamizwa nchini Myanmar.
-
UN kusaidia Waislamu Warohingya waliokimbia Myanmar
Sep 13, 2017 07:48Idadi ya Waislamu wa jamii Warohingya ambao wanakimbia mateso na mauaji huko Myanmar inaongezeka kila uchao katika hali ambayo, mashirika ya Umoja wa Mataifa na wadau wao wanaendelea kuhakikisha wanafikisha misaada ya dharura kwa wakimbizi hao ambao wengi wao ni Waislamu.
-
Nigeria yaitaka UN kusitisha maangamizi ya Waislamu wa Rohingya, Myanmar
Sep 12, 2017 15:03Nigeria imelaani maangamizi yanayofanyika nchini Myanmar dhidi ya jamii ya Waislamu wa Rohingya na kuutaka Umoja wa Mataifa kutekeleza majukumu yake na kusitisha operesheni za kijeshi za kuwahamisha kwa mabavu Waislamu wa jamii ya Rohingya.
-
Kiongozi Muadhamu: Ufumbuzi wa suala la Myanmar ni nchi za Kiislamu kuchukua hatua za kivitendo
Sep 12, 2017 07:56Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amekosoa kimya na kutochukua hatua jumuiya za kimataifa na wanaojigamba kuwa watetezi wa haki za binadamu kuhusiana na matukio ya maafa yanayojiri Myanmar na kusisitiza kwamba: Njia ya utatuzi wa kadhia hii ni kuchukuliwa hatua za kivitendo na nchi za Kiislamu na kuishinikiza kisiasa na kiuchumi serikali isiyo na huruma ya Myanmar.
-
Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu za Kiislamu yalaani mauaji dhidi ya Waislamu wa Myanmar
Sep 12, 2017 04:41Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu za Kiislamu imelaani vikali mauaji na jinai dhidi ya Waislamu Warohingya wa nchini Myanmar.