Pars Today
Wanajeshi saba wa Niger wameuawa baada ya kambi yao kushambuliwa na wanachama wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Boko Haram kusini mashariki mwa nchi karibu na mpaka wa Nigeria.
Siku moja baada ya raia 10 kuuawa kaskazini mashariki mwa Nigeria kufuatia shambulio la kigaidi, askari kumi waliokuwa katika operesheni ya pamoja wameuawa na watu waliokuwa wamebeba silaha katika mpaka wa nchi hiyo na Niger.
Machafuko katika maeneo ya mpaka wa Niger na nchi za Mali na Burkina Faso yamepelekea raia 52,000 wa Niger kuwa wakimbizi mwaka huu wa 2018.
Wasichana wasiopungua 18 wameripotiwa kutekwa nyara na watu waliokuwa wamejizatiti kwa silaha kusini mashariki mwa Niger.
Watu waliojizatiti kwa silaha wanaoaminika kuwa na mfungamano na genge la kigaidi na ukufurishaji la Boko Haram wameshambulia kampuni ya kuchimba visima vya maji ya Ufaransa ya Foraco kusini mashariki mwa Niger na kuua watu wasiopungua saba.
Raia zaidi ya 20 wa kabila la Tuareg nchini Mali wameuawa katika mpaka wa nchi hiyo na Niger, kufuatia mashambulio yaliyotekelezwa katika eneo moja kaskazini mashariki mwa nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika.
Umoja wa Mataifa umeripoti kuwa, watu wasiopungua 67 wamepoteza maisha kutokana na mripuko wa kipindupindu nchini Niger tokea mwezi Julai mwaka huu hadi sasa.
Ofisi ya kuratibu masuala ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa imetangaza kuwa, zaidi ya watu elfu 17 wamekimbia makazi yao huko magharibi mwa Niger tangu mwanzoni mwa mwaka huu wa 2018.
Wizara ya Afya ya Niger imesema kuwa, watu wasiopungua 22 wamepoteza maisha kutokana na mripuko mpya wa kipindupindu nchini humo.
Shirika la Kimataifa la Uhajiri limetangaza kuwa wahajiri zaidi ya 100 kutoka nchi za Afrika wameokolewa katika eneo la mpaka wa pamoja wa Niger na Algeria.