-
Nigeria yalaaniwa kwa kukandamiza waandamanaji wa Siku ya Quds
Mar 30, 2025 11:12Baraza la Uratibu wa Tablighi ya Kiislamu la Iran limetoa taarifa ya kulaani ukandamizaji waliofanyiwa Waislamu wa Nigeria wakati wa kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Quds na kuandika: "Ukandamizaji na kumwagwa damu za waandamanaji wa Siku ya Kimataifa ya Quds nchini Nigeria na kuuawa shahidi kidhulma Waislamu 18 waliokuwa kwenye saumu ya Ramadhani kunaonesha hofu ya watawala wa Nigeria kuhusu mwamko wa Waislamuj na nafasi ya kiistratijia ya Siku ya Kimataifa ya Quds duniani."
-
Magaidi washambulia kambi za jeshi Nigeria, Cameroon na kuua askari 16
Mar 27, 2025 11:08Watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa magenge ya kigaidi wamefanya mashambulizi yaliyoratibiwa dhidi ya kambi ya jeshi la Cameroon karibu na Ziwa Chad na dhidi ya kituo cha kijeshi kaskazini mashariki mwa Nigeria, na kuua takriban wanajeshi 16.
-
Nigeria yathibitisha vifo vipya vitano kutokana na homa ya Lassa
Mar 13, 2025 02:21Nigeria imethibitisha vifo vipya vitano kutokana na homa ya Lassa, ugonjwa ambao umesambaa katika eneo la magharibi mwa Afrika.
-
Mripuko wa homa ya uti wa mgongo waua makumi Nigeria
Mar 12, 2025 07:05Watu wasiopungua 26 wameaga dunia kutokana na mripuko wa ugonjwa wa uti wa mgongo (Meningitis) katika Jimbo la Kebbi kaskazini magharibi mwa Nigeria.
-
Sheikh Zakzkay: Muqawama umezaliwa upya nchini Lebanon
Feb 24, 2025 03:06Kiongozi wa Waislamu wa madhebeu ya Shia nchini Nigeria amesisitiza kuwa, kushiriki mamilioni ya watu katika mazishi ya Mashahidi wa Muqawama ni sawa na "kuzaliwa upya Muqawama wa Lebanon".
-
Abuja yaijia juu Canada kwa kumyima 'viza' Mkuu wa Jeshi la Nigeria
Feb 14, 2025 12:10Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Nigeria, Jenerali Christopher Musa, ameeleza kusikitishwa kwake na hatua ya ubalozi wa Canada katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi, kumnyima yeye na maafisa wengine wakuu wa kijeshi viza ya kwenda Canada kuhudhuria hafla ya michezo ya maveterani wa vita huko Vancouver.
-
Polisi ya Nigeria yakadhibisha kutoweka maelfu ya bunduki
Feb 13, 2025 11:20Jeshi la Polisi la Nigeria limekanusha ripoti kwamba maelfu ya silaha zimetoweka kwenye maghala yake ya silaha na kuitaja rupoti hiyo kuwa ni ya kupotosha na isiyo sahihi.
-
Wafanyabiashara Nigeria wataka kususiwa bidhaa za Israel
Feb 10, 2025 11:26Kundi moja la wajasiriamali wadogo na wa kati nchini Nigeria, limeandaa mkutano wa siku mbili katika Jimbo la Kaduna la kaskazini magharibi mwa nchi, kujadili mikakati ya kibiashara na umuhimu wa kususia bidhaa za Israel, ili kuonyesha uungaji mkono kwa kadhia ya Palestina.
-
Jeshi la Nigeria laangamiza magaidi 70 wa Boko Haram
Jan 27, 2025 12:25Wizara ya Ulinzi ya Nigeria imesema wanamgambo wasiopungua 70 wa Boko Haram waliuawa katika msururu wa operesheni za karibuni za kijeshi katika jimbo la Borno, kaskazini mashariki mwa nchi.
-
Makumi ya wanajeshi wa Nigeria wauawa katika shambulio la kigaidi
Jan 27, 2025 02:25Watu wanaoshukiwa kuwa magaidi wamewaua wanajeshi 20 wa Nigeria, akiwemo kkamanda wa ngazi ya juu, baada ya kushambulia kambi moja ya jeshi katika jimbo la Borno la kaskazini mashariki.