-
Waislamu Nigeria wataka kuachiwa huru kiongozi wa Palestina
Aug 29, 2025 02:24Harakati ya Kiislamu ya Nigeria imelaani vikali hatua ya polisi ya Nigeria kumkata kiongozi wa Jumuiya ya Wapalestina katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi, Ramzy Abu Ibrahim, ikisisitiza kuwa kukamatwa huko kunafungamana na makubaliano ya hivi karibuni ya usalama kati ya Nigeria na utawala wa Israel.
-
Kampuni ya Mafuta ya Serikali ya Nigeria: Wizi wa mafuta kupitia mabomba wakaribia kukomeshwa
Aug 26, 2025 02:45Kampuni ya mafuta ya serikali ya Nigeria (NNPC Limited) imeripoti kuwa karibu wizi wote wa mafuta uliokuwa ukifanywa kupitia mabomba umekaribia kukomeshwa, baada ya juhudi zilizoratibiwa na mashirika ya ulinzi na intelijensia ya nchi hiyo.
-
Je, ushirikiano wa kijeshi wa Marekani na Nigeria unaongeza hatari ya ukiukaji wa haki za binadamu?
Aug 25, 2025 05:53Hivi karibuni Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilitangaza kuwa ili kuisaidia Nigeria katika mapambano dhidi ya makundi ya kigaidi, imekubali kuiuzia nchi hiyo silaha zenye thamani ya takriban dola milioni 346.
-
Amnesty yaikosoa Nigeria kwa kuwakandamiza Waislamu wakiitetea Gaza
Aug 21, 2025 05:13Mkurugenzi wa shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty International nchini Nigeria, Isa Sunusi, amelaani vikali ukandamizaji mkali wa vyombo vya serikali dhidi ya Waislamu wa madhehebu ya Shia, wakati wa maandamano ya kulaani jinai za Israel dhidi ya Wapalestina wa Gaza, na kusema kuwa takriban wanachama 83 wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria bado wako rumande bila kufunguliwa mashtaka, licha ya kupata majeraha ya risasi na makovu mengineo wakishiriki maandamano ya amani.
-
Watu 27 wauawa katika shambulio la kigaidi msikitini Nigeria
Aug 20, 2025 06:46Magaidi waliokuwa na silaha jana Jumanne waliwauwa waumini karibu 27 waliokuwa msikitini katika jimbo la Katsina kaskazini magharibi mwa Nigeria.
-
Zakzaky: Mipango ya kuwafukuza Wapalestina Gaza, kuipokonya silaha Hizbullah itafeli
Aug 19, 2025 10:44Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria, Sheikh Ibrahim Yaqoub Zakzaky amebainisha kuwa, mipango ya utawala wa Kizayuni ya kuwaondoa kwa nguvu Wapalestina wa Ukanda wa Gaza katika ardhi yao na kuipokonya silaha Harakati ya Muqawama ya Hizbullah ya Lebanon kwa kutumia serikali ya Beirut itagonga mwamba.
-
Wanahabari Nigeria walaani mauaji ya waandishi wenzao huko Gaza
Aug 18, 2025 06:43Muungano wa Waandishi wa Habari wa Nigeria (NUJ) umelaani vikali mauaji ya wanahabari yaliyofanywa na utawala ghasibu wa Israel huko Gaza na kusisitiza kuwa, hujuma hizo za utawala wa Kizayuni dhidi ya waandishi wenzao katu haziwezi kuwazuia wahudumu wa tasnia hiyo kuendelea kufichua ukweli.
-
Operesheni ya pamoja ya AUSSOM na jeshi la Somalia yaangamiza zaidi ya magaidi 50 wa Al Shabab
Aug 04, 2025 11:02Vikosi vya Umoja wa Afrika vya Usaidizi na Kuleta Uthabiti nchini Somalia vimetangaza kuwa, zaidi ya magaidi 50 wa kundi la Al Shabab wameuawa katika operesheni ya pamoja iliyotekelezwa na vikosi hivyo na jeshi la Somalia (SNAF) katika mji wa Bariire, huko Lower Shabelle.
-
Jumapili, 03 Agosti, 2025
Aug 03, 2025 02:24Leo ni Jumapili tarehe 9 Mfunguo Tano Safar 1447 Hijria mwafaka na 3 Agosti 2025 Miladia.
-
Kufuatia hatua ya TZ, EAC yazitolea mwito nchi wanachama ziheshimu mpango wa soko la pamoja
Aug 01, 2025 07:17Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Veronica Nduva, amezitaka nchi wanachama za jumuiya hiyo kutekeleza mikataba yenye kuheshimu mpango wa soko la pamoja kwa ajili ya kufikia utangamano wa kikanda.