-
Utafiti: Vita vya mauaji ya kimbari vya Israel vimegharimu zaidi ya miaka milioni 3 ya maisha ya mwanadamu huko Gaza
Nov 05, 2025 03:06Utafiti wa hivi karibuni uliochapishwa katika jarida la Lancet umefichua kuwa zaidi ya miaka milioni tatu ya maisha ya binadamu yamepotea katika Ukanda wa Gaza tangu utawala ghasibu wa Israel uanzishe kampeni yake ya mauaji ya kimbari dhidi ya watu Ukanda wa Gaza ulio chini ya mzingiro, mwezi Oktoba mwaka 2023.
-
Nyaraka za jeshi la Israel zafichua: Mfungwa wa Kipalestina aliyebakwa alikuwa raia, si mpiganaji
Nov 04, 2025 11:18Waraka wa siri wa jeshi la Israel umefichua kwamba mtu aliyeshambuliwa kikatili na kubakwa na kundi la wanajeshi wa Israel katika gereza maarufu la Sde Teiman mnamo Julai mwaka jana hajawahi kushtakiwa kwa uhalifu wowote na alikuwa raia, kinyume na madai kwamba alikuwa na mwanachama harakati za mapambano ya Hamas.
-
Israel yaandaa muswada wa 'kifashisti' wa kuruhusu utoaji wa hukumu ya adhabu ya kifo kwa Wapalestina
Nov 04, 2025 02:25Kamati moja ya wabunge wa utawala wa kizayuni wa Israel imeidhinisha muswada wa kuanzisha utoaji wa adhabu ya kifo kwa Wapalestina wanaoshikiliwa kwenye magereza ya utawala huo, na kufungua njia ya kusomwa hoja hiyo kwa mara ya kwanza bungeni licha ya kuandamwa na lawama nyingi.
-
Israel yaendelea kuwatesa kwa njaa Wapalestina kwa kuruhusu 24% tu ya misaada kuingizwa Ghaza
Nov 02, 2025 06:50Mamlaka za Palestina katika Ukanda wa Ghaza zimetangaza kuwa utawala wa kizayuni wa Israel umeruhusu kuingizwa katika eneo hilo sehemu ndogo tu ya misaada ya kibinadamu kinyume na ilivyoafikiwa katika makubaliano ya usitishaji mapigano yanayosimamiwa na serikali ya Marekani, ambayo yalianza kutekelezwa mwezi uliopita.
-
UNICEF: Usitishaji vita Gaza ni fursa muhimu ya kukidhi mahitaji ya watoto
Oct 28, 2025 03:14Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) umetangaza kuwa, usitishaji vita katika Ukanda wa Gaza unaweza kuwa "fursa muhimu" ya kulinda maisha, utu na mahitaji muhimu ya watoto milioni moja wa Kipalestina.
-
Hamas yasisitiza haki ya Wapalestina ya kuwa na nchi huru; yasema imesitisha mapigano Gaza
Oct 27, 2025 06:28Afisa wa ngazi ya juu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) amesisitiza dhamira isiyoyumba ya harakati hiyo ya kutekeleza usitishaji vita huko Gaza na kusema Wapalestina hawataki kitu chochote isipokuwa haki yao inayotambulika kimataifa ya kuwa na nchi huru.
-
MSF: Israel inaendelea kutumia misaada ya Gaza kama silaha ya vita
Oct 27, 2025 02:43Afisa mkuu wa shirika la kimataifa la misaada ya kibinadamu la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) anasema utawala wa Israel unaendelea kutumia misaada ya kibinadamu huko Gaza kama silaha ya vita dhidi ya Wapalestina.
-
Kwa nini UNRWA huko Gaza inalengwa kwa mashinikizo ya kisiasa?
Oct 26, 2025 06:09Mkuu wa Shirika la Misaada na Ajira kwa Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) amesema: Vita vya Gaza vimeonyesha kwamba sheria za kimataifa hazizingatiwi kabisa.
-
Ripoti: Asilimia 97 ya shule za Gaza zimeharibiwa kwa mashambulizi ya Israel
Oct 20, 2025 03:28Ripoti rasmi zinasema, mashambulizi ya utawala ghasibu wa Israel yameharibu asilimia 97 ya shule za Ukanda wa Gaza na hivyo kuhatarisha mustakbali wa kielimu wa wanafunzi laki tatu wa Kipalestina katika eneo hilo.
-
HAMAS: Hatutajifunga kukabidhi silaha mpaka yatakapofanyika mazungumzo zaidi
Oct 19, 2025 02:42Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imesisitiza kuwa haitajifunga moja kwa moja kukabidhi silaha na inatumai usitishaji vita na utawala wa kizayuni wa Israel utadumu kwa muda wa miaka mitatu hadi mitano ili kuijenga upya Ghaza.