-
EU yakosoa mpango wa Israel wa kujenga vitongoji vipya Ukingo wa Magharibi
Feb 29, 2020 09:50Umoja wa Ulaya umekosoa vikali mpango wa utawala wa Kizayuni wa Israel wa kujenga maelfu ya vitongoji vipya vya walowezi wa Kizayuni katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu na utawala huo ghasibu.
-
Risasi za jeshi la Israel zawapofusha Wapalestina 21 Ukanda wa Gaza
Feb 27, 2020 09:41Kituo cha Haki za Binadamu cha Beytulahm (Bethlehem) huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu kimeripoti kuwa, Wapelestina 21 katika Ukanda wa Gaza wamesababishiwa upofu na ufyatuaji risasi wa jeshi katili la utawala wa Kizayuni wa Israel ndani ya miaka miwili iliyopita.
-
Baraza la Usalama la UN launga mkono suala la kuundwa nchi huru ya Palestina
Feb 26, 2020 01:03Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetangaza uungaji mkono wake kamili kwa suala la kuundwa nchi huru ya Palestina na kuendelezwa "mazungumzo yenye itibari" baina ya pande mbili.
-
Utawala wa Kizayuni watishia kuwaua kigaidi viongozi wa Palestina huko Ukanda wa Ghaza
Feb 25, 2020 10:02Viongozi wa utawala wa Kizayuni wametishia kuwaua kigaidi viongozi wa Harakati za Muqawama wa Kiislamu za Palestina za Hamas na Jihadul Islami huko Ukanda wa Ghaza.
-
Rais wa Tunisia: Quds ni mji mkuu wa Palestina, si bidhaa ya kuuzwa
Feb 25, 2020 04:18Rais Kais Saied wa Tunisia amesema Palestina ni milki ya Wapalestina na Quds tukufu inapaswa kuwa mji mkuu wa taifa hilo la Kiarabu.
-
Mashambulizi mapya ya Israel dhidi ya Wapalestina, matunda ya mwanzo ya "Muamala wa Karne"
Feb 24, 2020 08:52Ikiwa haujapita mwezi mmoja sasa tangu Rais Donald Trump wa Marekani alipozindua rasmi mpango uliopewa jina la "Muamala wa Karne", utawala wa Kizayuni wa Israel umeanzisha duru mpya ya vita na mashambulizi dhidi ya makundi na harakati za kupigania ukombozi za Palestina.
-
Papa Francis akosoa mpango wa Trump wa Muamala wa Karne
Feb 24, 2020 01:10Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, kwa njia isiyo ya moja kwa moja amekosoa mpango wa Rais Donald Trump wa Muamala wa Karne ambapo ameonya kuwa, mipango ya namna hiyo inayoegemea upande mmoja haiwezi kuupatia ufumbuzi mgogoro wa Palestina na Israel.
-
Wapalestina kadhaa wauawa shahidi na wanajeshi wa Israel Ukanda wa Gaza
Feb 23, 2020 09:58Askari wa jeshi katili la utawala wa Kizayuni wa Israel wamewapiga risasi na kuwaua shahidi Wapalestina wawili katika uzio unaotenganisha Ukanda wa Gaza na ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Israel.
-
Umoja wa Ulaya: Tunaunga mkono kuundwa nchi huru ya Palestina
Feb 22, 2020 09:10Josep Borrell, Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya amesisitiza kuwa, umoja huo unaunga mkono juhudi zinazofanyika kwa ajili ya kuundwa nchi huru ya Palestina.
-
Seneti ya Pakistan yapasisha azimio dhidi ya njama ya Trump ya "Muamala wa Karne"
Feb 20, 2020 04:45Baraza la Seneti la Pakistan limepasisha kwa sauti moja azimio linalopinga mpango wa Rais Donald Trump wa Marekani kuhusu Palestina uliopewa jina la "Muamala wa Karne" likisema kuwa unawataka Wapalestina wasalimu amri kwa utawala wa Kizayuni wa Israel.