-
Larijani: Israel inafanya njama za kuzusha vurugu za kisiasa katika Mashariki ya Kati
Dec 18, 2017 10:44Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, utawala dhalimu wa Israel unafanya njama za kuleta vurugu za kisiasa katika Mashariki ya Kati na kuongeza kuwa, endapo nchi za Kiislamu zitadumisha umoja na mshikamano zitazuia kufikiwa malengo hayo ya Wazayuni.
-
Utawala wa Kizayuni na utumiaji wa gesi za sumu dhidi ya Wapalestina
Dec 18, 2017 08:00Kitendo cha kiuadui cha rais wa Marekani, Donald Trump cha kuitangaza Quds tukufu kuwa eti ni mji mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel kimekiuka sheria na makubaliano yote ya kimataifa na kuandaa uwanja wa kufutwa kikamilifu taifa la Palestina katika uso wa dunia.
-
Saudia yapanga uhaini mwingine, mara hii ni kuiuzia Israel maeneo ya Palestina, Quds Tukufu ikiwemo
Dec 18, 2017 01:13Tovuti ya Intaneti ya Arabi 21 imefichua kuwa, mrithi wa ufalme wa Saudia anapanga njama kubwa ambayo mara hii inajumuisha kuiuzia Israel eneo la Palestina la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na mji wa Quds Tukufu (Jerusalem) uliko Msikiti wa Al Aqsa kwa mabilioni ya dola.
-
Kikao cha dharura cha kamati ya Palestina ya Muungano wa Mabunge ya Kiislamu kufanyika kesho Tehran
Dec 17, 2017 10:43Kikao cha dharura cha kamati ya Palestina ya Muungano wa Kimataifa wa Mabunge ya nchi za Kiislamu kinatarajiwa kufanyika kesho hapa mjini Tehran kwa kuhudhuriwa na Maspika wa Mabunge ya nchi tatu za Iran, Mali na Iraq.
-
Huenda Baraza la Usalama la UN likakutana kesho kujadili uamuzi wa Trump dhidi ya Quds
Dec 16, 2017 04:41Mwakilishi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa amesema, kuna uwezekano kikao cha dharura cha Baraza la Usalama la umoja huo kikafanyika hapo kesho kujadili rasimu ya azimio linalohusu uamuzi uliochukuwa na Marekani dhidi ya mji wa Baitul Muqaddas.
-
Tunisia yabadilisha jina la vituo vya TAXI na kuita Quds
Dec 15, 2017 00:48Chama cha wamiliki wa TAXI nchini Tunisia kimebadilisha jina la vituo vyake na kuviita Quds kama njia ya kulalamikia uamuzi wa Marekani wa kuitambua rasmi Quds kuwa eti ni mji mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Hamas: Hakuna nchi inayoitwa 'Israel' hata mji mkuu wake uwe 'Quds'
Dec 14, 2017 12:31Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina Hamas imelaani vikali uamuzi wa Rais wa Marekani, Donald Trump wa kuitangaza Baytul Muqaddas kuwa mji mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel na kusisitiza kuwa, hakuna dola linaloitwa Israel hata mji mkuu wake uwe Quds tukufu.
-
Mwakilishi wa Mayahudi katika bunge la Iran: Hatua ya Trump ya kuitambua Quds mji mkuu wa Israel ni ubaguzi wa kimbari
Dec 14, 2017 12:29Mwakilishi wa jamii ya wachache ya Mayahudi katika Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran amesema hatua ya rais wa Marekani ya kuitangaza Baitul Muqaddas mji mkuu wa utawala wa Kizayuni ni ubaguzi wa kimbari.
-
Erdogan: Israel ni dola vamizi na la kigaidi
Dec 13, 2017 12:43Rais Recep Tayyip Erdoğan wa Uturuki amesema kuwa, kuwa na nguvu na kumiliki silaha si dalili kuwa Marekani ina nguvu, na maamuzi yake yatasababisha matatizo makubwa katika eneo la Mashariki ya Kati.
-
Jumuiya ya NAM yakosoa hatua ya Marekani dhidi ya Quds
Dec 13, 2017 11:55Jumuiya ya Nchi Zisizofungamana na Siasa za Upande Wowote (NAM) imekosoa vikali hatua ya Rais Donald Trump wa Marekani ya kuitambua Quds kuwa eti mji mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel.