-
Rais Rouhani: Taifa la Iran litalipiza kisasi cha kuuliwa kigaidi, shahid Fakhrizadeh
Nov 28, 2020 11:47Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, maadui wote watambue kwamba, wananchi na viongozi wa Iran ni mashujaa na wenye ghera kubwa, hivyo lazima watalipiza kisasi cha vitendo vya jinai linavyofanyiwa taifa hili la Kiislamu.
-
Rais Rouhani: Mauaji ya wanasayansi wa nyuklia yanatokana na maadui kushindwa mtawalia
Nov 28, 2020 08:07Rais Hassan Rouhani amesema, hapana shaka tukio la kigaidi na la kutapatapa la mauaji ya wanasayansi wa nyuklia linatokana na kushindwa na kuemewa maadui waliolikamia taifa la Iran.
-
Rais Rouhani: Iran inaweza kuyadhaminia mataifa ya dunia mahitaji yao kwa bei rahisi zaidi
Nov 26, 2020 11:44Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Tehraninao uwezo wa kulidhaminia eneo hili na hata dunia nishati ya bei rahisi zaidi
-
Rouhani: Nia ya Iran ni kuwa na uhusiano wa kiudugu na nchi za pembezoni mwa Ghuba ya Uajemi
Nov 26, 2020 03:54Rais Hassan Rouhani amesema uhusiano wa Iran na Qatar ni wa kirafiki na unaendelea kustawi na akasisitiza kwamba inachotaka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kuwa na mazungumzo, maelewano na uhusiano wa kiudugu na nchi za pembezoni mwa Ghuba ya Uajemi.
-
Rais Rouhani: Serikali ijayo ya Marekani ifidie makosa yaliyotangulia
Nov 25, 2020 12:19Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria ushindi wa wananchi wa Iran na kushindwa adui katika vita vyake vya kiuchumi dhidi ya taifa hili na kueleza kwamba, serikali ijayo ya Marekani inapaswa kulaani waziwazi sera na hatua zisizo za kibinadamu na kigaidi za Donald Trump na ifidie siasa hizo zisizo sahihi.
-
Rouhani: Utawala wa sasa wa Marekani ni wa kijinai na kigaidi
Nov 18, 2020 12:01Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria kuhusu mienendo haribifu na ugaidi wa kiuchumi wa Washington na kusema kuwa, utawala ulioko madarakani hivi sasa nchini Marekani ni mtenda jinai na dola la kigaidi.
-
Rouhani: Bajeti ijayo ya Iran haitategemea mapato ya mafuta
Nov 15, 2020 13:00Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema muswada wa bajeti ya mwaka ujao wa kifedha wa Iran unapania kufuta kikamilifu utegemezi wa mapato ya mauzo ya mafuta.
-
Rais Rouhani: Mashinikizo ya kiwango cha juu yanaelekea ukingoni
Nov 12, 2020 10:38Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa mashinikizo ya kiwango cha juu ya Marekani yanaelekea ukingoni na kuongeza kuwa, taifa la Iran hivi karibuni litavuna matunda ya kusimama kwake kidete na imara mbele ya mashinikizo hayo.
-
Rais Ruouhani: Kudhamini amani ya eneo na kuheshimu haki za mataifa ni katika siasa thabiti za Iran
Nov 11, 2020 15:08Rais Hassan Rouhani amesema, kudhamini amani na uthabiti wa eneo, kuheshimu haki za mataifa, kutoingilia masuala ya ndani ya nchi zingine, kupambana na ugaidi, kuhitimisha mielekeo ya uchukuaji hatua za upande mmoja, kutekeleza makubaliano na kuwa na maelewano chanya ni miongoni mwa siasa na sera zisizobadilika za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Rais Rouhani: Serikali mpya ya Marekani irekebishe sura yake mbaya katika mahusiano na nchi nyingine
Nov 10, 2020 11:58Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa serikali mpya ya Marekani inapaswa kufanya marekebisho katika mienendo yake isiyo ya kibinadamu na nchi nyingine za dunia.