Rais Rouhani: Mashinikizo ya kiwango cha juu yanaelekea ukingoni
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i64581-rais_rouhani_mashinikizo_ya_kiwango_cha_juu_yanaelekea_ukingoni
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa mashinikizo ya kiwango cha juu ya Marekani yanaelekea ukingoni na kuongeza kuwa, taifa la Iran hivi karibuni litavuna matunda ya kusimama kwake kidete na imara mbele ya mashinikizo hayo.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Nov 12, 2020 10:38 UTC
  • Rais Hassan Rouhan
    Rais Hassan Rouhan

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa mashinikizo ya kiwango cha juu ya Marekani yanaelekea ukingoni na kuongeza kuwa, taifa la Iran hivi karibuni litavuna matunda ya kusimama kwake kidete na imara mbele ya mashinikizo hayo.

Rais Rouhani ameyasema hayo mapema leo katika uzinduzi wa miradi kadhaa ya elimu na matibabu uliofanyika kwa njia ya video. Amesema kuwa, vielelezo vyote duniani, kuanzia Marekani hadi katika nchi nyingine, vinaonyesha kuwa, mashinikizo ya kiwango cha juu yamefeli na yanaelekea ukingoni. 

Rais Hassan Rohani amesema anatarajia kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itavuka salama kipindi kigumu cha vikwazo vya kidhalimu na vinavyokiuka sheria vya maadui kwa msaada wa taasisi zote za utendaji na msaada wa wananchi.

Rais Hassan Rouhani

Ameashiria uzinduzi wa miradi kadhaa ya masuala ya tiba na afya na kusema: Hii leo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inahesabiwa kuwa miongoni mwa nchi zilizopiga hatua kubwa katika masuala ya elimu ya tiba na taaluma ya udaktari, na idadi kubwa ya wagonjwa kutoka maeneo mbalimbali ya dunia wanakuja hapa nchini kupata huduma za tiba kutokana na kuwa na madaktari bingwa na wachapakazi.