Iran yatahadharisha kuhusu Marekani kulitumia vibaya Baraza la Usalama la UN
-
Amir Saeed Iravani
Mwakilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa ameeleza kuwa: "Marekani inalitumia vibaya Baraza la Usalama kwa kueneza uwongo na tuhuma zisizo na msingi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na mpango wake wa nyuklia."
Amir Saeed Iravani ameeleza kuwa: Marekani ni nchi pekee katika historia ambayo imetumia silaha za nyuklia huku ikishambulia vituo vya amani vya nyuklia vilivyo chini ya usimamizi na ukaguzi wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Nyuklia (IAEA). Marekani aidha inashambulia raia na miundombinu yao na kuendelea kukiuka sheria za kimataifa kupitia mzingiro haramu wa baharini huku ukiunga mkono kwa pande zote jinai na maafa yanayosababishwa na uhalifu wa utawala wa Kizayuni wa Israel katika kanda hii.
Mwakilishi wa Jamhuri ya Kiislamu UN ameongeza kuwa: Marekani kwa mara nyingine imelitumia vibaya jukwaa la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kueneza uwongo, kuta tuhuma zisizo na msingi na kusambaza habari za kupotosha dhidi ya Iran na mpango wake wa amani wa nyuklia.
Mwakilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amesisitiza kuwa: "Kwa hakika, mhalifu na mwizi hivi sasa anatekeleza nafasi ya mwendesha mashtaka na hakimu; na anajaribu kuficha jinai zake."