Rouhani: Bajeti ijayo ya Iran haitategemea mapato ya mafuta
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i64643-rouhani_bajeti_ijayo_ya_iran_haitategemea_mapato_ya_mafuta
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema muswada wa bajeti ya mwaka ujao wa kifedha wa Iran unapania kufuta kikamilifu utegemezi wa mapato ya mauzo ya mafuta.
(last modified 2025-11-12T06:10:22+00:00 )
Nov 15, 2020 13:00 UTC
  • Rouhani: Bajeti ijayo ya Iran haitategemea mapato ya mafuta

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema muswada wa bajeti ya mwaka ujao wa kifedha wa Iran unapania kufuta kikamilifu utegemezi wa mapato ya mauzo ya mafuta.

Rais Rouhani amesema hayo katika Mkutano wa 181 uliofanyika katika Makao Makuu ya Uratibu wa Uchumi hapa Tehran na kuongeza kuwa, bajeti ijayo ya nchi hii inaazimia kubana matumizi na kuongeza mapato, ili kwa utaratibu huo, ipunguze nafasi ya serikali katika ukuaji wa uchumi.

Amesema muswada wa bajeti ya mwaka ujao wa kifedha wa Iran utajikita zaidi katika ustawi wa muda mrefu kupitia mauzo ya bidhaa nyinginezo ghairi ya mafuta, uongeze jitihada katika vita dhidi ya janga la corona na kupunguza taathira zake kwa uchumi wa nchi, kupiga jeki shughuli za kibiashara, na kutoa kipaumbele katika kupunguza gharama za maisha ya wananchi wa Iran.

Vikwazo vya US dhidi ya Iran hata katika kipindi hiki cha corona

Rais wa Iran amesisitiza kuwa, kuendesha nchi hii bila ya kutegemea sana mapato ya mauzo ya mafuta ni kielelezo cha nguvu kubwa ya Iran katika medani ya vita vya kiuchumi.

Dakta Rouhani ameeleza bayana kuwa, maadui walidhani kwamba ustawi wa kiuchumi wa Iran ungesimama baada ya kuanzisha vikwazo dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu, lakini hii leo nchi hii inaendeshwa kwa mipango mizuri bila ya kutegemea mapato ya mafuta