-
Qatar: Saudia inaendesha kisiasa Ibada ya Hijja
Jul 30, 2017 10:43Kamisheni Taifa ya Haki za Binadamu nchini Qatar imelalamikia vikali uendeshaji wa kisiasa wa ibada tukufu ya Hijja unaofanywa na utawala wa Aal-Saud wa Saudi Arabia.
-
Waingereza wapatwa na wasi wasi kwa hatua ya Msaudia kununua hisa za intaneti nchini kwao
Jul 29, 2017 22:35Kitendo cha muwekezaji mmoja wa Saudia cha kununua sehemu kubwa ya hisa za tovuti ya gazeti la Independent ya nchini Uingereza, kimeyatia wasi wasi mkubwa makundi ya watetezi wa haki za binaadamu na uhuru wa vyombo vya habari vya taifa hilo.
-
Saudia na Imarati zinajiandaa kuweka wazi mahusiano yao na utawala wa Kizayuni
Jul 29, 2017 09:14Sambamba na kuwepo mahusiano ya muda mrefu kati ya nchi zinazolizingira kwa kila upande taifa la Qatar na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel, habari zinaarifu kwamba Saudia na Imarati zinajiandaa kuweka wazi mahusiano hayo kwa walimwengu.
-
Vikosi vya jeshi la Yemen vyateka vituo kadhaa vya jeshi la Saudia
Jul 29, 2017 03:23Jeshi la Yemen limeviteka vituo kadhaa vya jeshi la Saudi Arabia katika mkoa wa kusini magharibi mwa nchi hiyo wa Jizan.
-
London yakaribisha juhudi za Doha za kupunguza mivutano kati yake na nchi za Kiarabu
Jul 24, 2017 02:47Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza amekaribisha juhudi za serikali ya Qatar za kupunguza mivutano kati yake na nchi za Kiarabu za eneo la Ghuba ya Uajemi.
-
Imarati na Saudia zakataa wito wa Qatar wa mazungumzo
Jul 23, 2017 09:37Umoja wa Falme za Kiarabu umekataa wito uliotolewa hivi karibuni na Amir wa Qatar, Sheikh Tamin bin Hamad al-Thani, wa kufanyika mazungumzo ya kuupatia ufumbuzi mgogoro uliopo, na kusisitiza kuwa Doha sharti ibadili sera zake kabla ya kufanyika jitihada zozote za kuiondolea vikwazo nchi hiyo ndogo ya Ghuba ya Uajemi, iivyowekewa na Saudia na wapambe wake.
-
Mapinduzi ndani ya utawala wa kifalme Saudia yaendelea, mtoto mdogo wa Mfalme Salman ateuliwa kuwa balozi wa Riyadh huko Marekani
Jul 23, 2017 03:03Ndugu yake mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudi Arabia na mtoto mdogo wa Mfalme wa sasa wa nchi hiyo usiku wa kuamkia leo amekabidhi hati zake za utambulisho kwa Rais Donald Trump wa Marekani kama balozi mpya wa Saudia nchini humo.
-
Kuanzishwa taasisi mpya ya usalama na kuzidi kujiimarisha Mohammed bin Salman nchini Saudia
Jul 22, 2017 01:24Mfalme Salman bin Abdulaziz Aal Saud wa Saudi Arabia Alkhamisi usiku alitoa amri ya kuundwa taasisi mpya ya usalama nchini humo suala ambalo linahesabiwa na wachambuzi wa mambo kwamba limefanyika kwa nia ya kumtia nguvu mwanawe yaani Mohammed bin Salman, mrithi mpya wa kiti cha ufalme wa nchi hiyo.
-
Ugonjwa wa kipindupindu Yemen ni mbaya zaidi katika historia ya dunia
Jul 21, 2017 21:59Shirika la kutoa misaada la Oxfam linasema mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu Yemen ni mbaya zaidi katika historia ya zama hizi duniani. Kipindupidu kimeenea Yemen kufuatia hujuma ya kijeshi na mzingiro wa Saudia dhidi ya nchi hiyo.
-
Kuua wapinzani, silaha ya kisiasa inayotumiwa kwa ajili ya malengo ya kimadhehebu Saudi Arabia
Jul 20, 2017 03:09Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limekutaja kuua raia kuwa ni silaha ya kisiasa inayotumiwa na utawala wa Saudi Arabia kwa ajili ya kuwanyamazisha wapinzani wake.