Saudia yawafukuza maelfu ya vibarua Waethoipia kutokana na matatizo ya kiuchumi
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i32600-saudia_yawafukuza_maelfu_ya_vibarua_waethoipia_kutokana_na_matatizo_ya_kiuchumi
Utawala wa Aal Saud umewafukuza maelfu ya wafanyakazi za vibarua raia wa Ethiopia kutokana na matatizo ya kifedha yanayoikabili nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 02, 2017 09:51 UTC
  • Saudia yawafukuza maelfu ya vibarua Waethoipia kutokana na matatizo ya kiuchumi

Utawala wa Aal Saud umewafukuza maelfu ya wafanyakazi za vibarua raia wa Ethiopia kutokana na matatizo ya kifedha yanayoikabili nchi hiyo.

Utawala wa Saudia unatekeleza mpango wa kuwafukuza wafanyakazi za vibarua raia wa kigeni ambapo hadi sasa maelfu ya vibarua wameshafukuzwa nchini humo. Kwa mujibu wa maafisa wa utawala wa Riyadh, kuna wafanyakazi za vibarua laki nne wanaofanya kazi nchini Saudi Arabia kinyume cha sheria.

Mashirika ya kimataifa ya haki za binadamu yamewahi mara kadhaa kuzikosoa nchi za Kiarabu za pembezoni mwa Ghuba ya Uajemi na hasa Saudia kutokana na kuamiliana vibaya na vibarua wa kigeni. Kituo cha takwimu nchini Saudi Arabia kimetangaza hivi karibuni kuwa zaidi ya watu laki tisa na elfu sita hawana ajira nchini humo, nusu yao wakiwa ni wahitimu wa vyuo vikuu.

Vibarua raia Ethiopia baada ya kutiwa nguvuni nchini Saudia

Hivi sasa wastani wa ukosefu wa ajira nchini Saudia katika kipindi cha miezi mitatu ya mwanzo ya mwaka hu wa 2017 ni karibu asilimia saba. Hatua ya utawala wa Aal Saud ya kuanzisha vita vamizi dhidi ya Yemen na uungaji mkono wake kwa makundi ya kigaidi katika eneo hili la Mashariki ya Kati vimeutia hasara kubwa kifedha utawala huo wa kifalme.../