Pars Today
Waziri Mkuu wa Serikali ya Uokovu wa Kitaifa ya Yemen ameutaja muungano vamizi unaoongozwa na Saudi Arabia na Umoja wa Mataifa kuwa zinahusika katika kufeli kwa usitishaji vita huko Yemen.
Takriban wiki moja baada ya ziara ya Kansela wa Ujerumani Olaf Schultz nchini Saudi Arabia, Berlin kwa mara nyingine tena imeanza kuiuzia Saudia Arabia silaha na zana za kivita.
Chama cha mrengo wa kushoto cha Ujerumani kimekosoa vikali hatua ya serikali mpya ya muungano ya nchi hiyo ya kutoa leseni ya kuuza silaha kwa serikali ya Saudi Arabia.
Shirika la kutetea haki za binadamu la "Sanad" limetangaza kuwa kumeshuhudiwa ongezeko la kukamatwa wakosoaji na hukumu za kikatili na kidhalimu nchini Saudi Arabia katika kipindi cha hivi karibuni.
Shirika la Kimataifa la Kupambana na Mateso limesema katika ripoti yake kwamba, muungano vamizi unaoongozwa na Saudi Arabia ndio chimbuko la ukame na njaa inayowakabili wananchi wa Yemen kutokana na kuiziingira nchi nchi hiyo.
Makumi ya watetezi wa haki za binadamu wamefanya maandamano nje ya ubalozi wa Saudi Arabia mjini London, kulaani safari ya Mrithi wa Ufalme wa Saudi Arabia, Mohammed bin Salman nchini Uingereza.
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema ubunifu na hatua za Iraq katika kuboresha ushirikiano baina ya nchi za eneo bila uingiliaji wa madola ajinabi ni jambo ambalo limekuwa na taathira na kuongeza kuwa: "Kurekebishwa na kuimarishwa uhusiano wa Iran na Saudi Arabia ni kwa maslahi ya usalama wa eneo."
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iraq amesema, kikao kijacho cha Saudi Arabia na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Baghdad kitakuwa cha mazungumzo ya wazi kutokana na ombi lililotolewa na mrithi wa ufalme wa Saudia.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameipongeza Iraq kwa nafasi yake athirifu na jitihada zake za kushajiisha utumiaji wa mazungumzo kwa ajili ya kujaribu kutatua matatizo na changamoto zinaolikabili eneo hili la Asia Magharibi.
Hizbullah ya Lebanon imesema, hatua ya Saudi Arabia ya kuufungulia utawala haramu wa Kizayuni wa Israel mipaka ya anga yake ni sawa na kuwa mshirika wa jinai zinazofanywa na utawala huo na ni usaliti kwa umma wa Kiislamu.