Jul 18, 2022 08:02 UTC
  • Iran yaipongeza Iraq kwa kushajiisha mazungumzo katika eneo

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameipongeza Iraq kwa nafasi yake athirifu na jitihada zake za kushajiisha utumiaji wa mazungumzo kwa ajili ya kujaribu kutatua matatizo na changamoto zinaolikabili eneo hili la Asia Magharibi.

Katika mazungumzo na mwenzake wa Iraq kwa njia ya simu jana Jumapili, Hossein Amir-Abdollahian, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameishukuru serikali ya Baghdad kwa juhudu zake za kuanzisha mazungumzo ya kieneo, kwa shabaha ya kuimarisha usalama katika kanda hii ya kistratejia.

Amir-Abdollahian na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iraq, Fuad Hussein wamejadili uhusiano wa pande mbili wa Tehran na Baghdad, na masuala ya kieneo na kimataifa, yakiwemo mazungumzo ya Saudi Arabia na Jamhuri ya Kiislamu.

Mwanadiplomasia huyo wa ngazi ya juu wa Iran amesema, Tehran ipo tayari kuendelea na mashauriano na kubadishana mawazo na mwenzake wa Iraq, kwa ajili ya kufuatilia masuala yenye maslahi ya pamoja ya pande mbili na kieneo.

Kadhalika Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amemnyooshea mwenzake wa Iraq mkono wa kheri na fanaka, kwa minasaba ya sikukuu ya Ghadir Khum inayoadhimishwa leo, na Iddul Adh'ha iliyosherehekewa siku chache zilizopita.

Bendera za Iraq na Iran

Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iraq, Fuad Hussein sanjari na kumpongeza mwenzake wa Iran kwa ajili ya minasaba hiyo ya kidini, lakini amemtaarifu pia kuhusu tathmini yake juu ya mkutano wa juzi wa Jeddah, ambapo Baghdad iliwakilishwa.

Amesema Baghdad itaendelea kusisitizia haja ya kutumiwa njia za diplomasia na mazungumzo, kwa ajili ya kutatua matatizo ya kieneo na kuimarisha ushirikiano wa pande mbili na pande kadhaa miongoni mwa nchi za eneo, kwa ajili ya amani na uthabiti.

Tags