Kiongozi Mkuu: Jamhuri ya Kiislamu imebatilisha mantiki potofu ya Magharibi kuhusu mwanamke
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i133886-kiongozi_mkuu_jamhuri_ya_kiislamu_imebatilisha_mantiki_potofu_ya_magharibi_kuhusu_mwanamke
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ameashiria mwenendo wa Magharibi wa kukazania kueneza utamaduni wake potofu duniani na kueleza kwamba: "wao wanadai kuwa mipaka maalumu iliyowekwa kwa ajili ya mwanamke, ikiwemo hijabu, vitazuia maendeleo yake,
(last modified 2025-12-03T16:38:35+00:00 )
Dec 03, 2025 14:03 UTC
  • Kiongozi Mkuu: Jamhuri ya Kiislamu imebatilisha mantiki potofu ya Magharibi kuhusu mwanamke

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ameashiria mwenendo wa Magharibi wa kukazania kueneza utamaduni wake potofu duniani na kueleza kwamba: "wao wanadai kuwa mipaka maalumu iliyowekwa kwa ajili ya mwanamke, ikiwemo hijabu, vitazuia maendeleo yake,

lakini Jamhuri ya Kiislamu imebatilisha mantiki hii potofu na kuonyesha kwamba wanawake Waislamu walioshikamana na vazi la stara la Kiislamu, wanaweza kusonga mbele na kutoa mchango zaidi katika nyanja zote kuliko wanawake wengine".

Ayatullah Khamenei, ameyasema hayo leo mbele ya hadhara ya maelfu ya wanawake na wasichana kutoka maeneo mbalimbali nchini waliokwenda kumtembelea katika Husainiya ya Imam Khomeini (MA).

Katika mkutano huo, Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu amemuelezea Bibi Fatimatu-Zahra (SA) kuwa ni mwanadamu wa ulimwengu wa Malakuti aliyepambika kwa sifa tukufu za juu kabisa katika nyanja zote na huku akibainisha mtazamo wa Uislamu kuhusu hadhi na haki za wanawake kwa upande wa ndani ya nyumba na katika jamii, ameeleza mambo ya kufanywa na yasiyopasa kufanywa katika mwenendo ambao wanaume wanapaswa kuwa nao katika kuamiliana na wake zao na wanawake kwa ujumla katika nyanja mbalimbali.

Akiashiria sifa zisizo na upeo na ukomo za Bibi huyo mtukufu zaidi wa Ulimwengu wa Duniani na Akhera katika "ibada na unyenyekevu, kujitolea mhanga, usamehevu kwa watu, ustahamilivu katika shida na masaibu, kutetea kishujaa haki za wanaodhulumiwa, kuweka wazi na kubainisha haki na ukweli, uelewa na utendaji wa kisiasa, utekelezaji wa majukumu ya ndani ya nyumba, ya mke kwa mume na ya malezi ya watoto, kujitokeza katika matukio muhimu ya historia ya mwanzoni mwa Uislamu" na katika nyuga nyingine, Ayatullah Khamenei amesema: "Alhamdulillah, mwanamke wa Kiirani anafuata kigezo na mafunzo kutoka kwenye jua kama hili na kupiga hatua kwa kufuata malengo yake yeye, ambaye kwa mujibu wa kauli ya Mtume (SAW), ni Siti wa wanawake wote wa ulimwengu katika zama zote za historia".

Hadhara ya akina mama na wasichana wakisikiliza hotuba ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu

 

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema, hadhi ya wanawake katika Uislamu ni tukufu na ya juu mno na akaongeza kwamba: "tafsiri inayotoa Quran kuhusu utambulisho na shakhsia ya mwanamke ni ya juu zaidi kiutukufu na ya kimaendeleo zaidi."

Ayatullah Khamenei ameashiria Aya za Quran Tukufu kuhusu "nafasi sawa ya mwanamke na mwanamume katika maisha na historia ya mwanadamu, na fursa sawa kwa mwanamke na mwanamume katika ujengekaji ili kufikia ukamilifu wa kiroho na nafasi za juu za utukukaji," na akasema: "mambo haya yote yanapingana na watu walio na dini lakini wenye ufahamu usio sahihi wa dini, na wale ambao kimsingi hasa hawaikubali dini."

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema, kwa mtazamo wa Uislamu, utamaduni potofu wa Magharibi na ubepari havikubaliki kikamilifu; na akafafanua kwa kusema: ili kulinda hadhi ya wanawake na kudhibiti matamanio yenye nguvu kubwa sana na hatari ya kingono, katika Uislamu kuna mipaka na hukumu kuhusu "mahusiano kati ya mwanamke na mwanamume, uvaaji wa mwanamke na mwanamume, hijabu ya mwanamke na ushajiishaji wa ndoa," ambayo yanaendana kikamilifu na maumbile ya mwanamke na maslahi na mahitaji halisi ya jamii; ilhali kudhibiti matamanio ya ngono yasiyo na mwisho na haribifu katika utamaduni wa Magharibi hakuzingatiwi hata kidogo.

Ayatullah Khamenei amesema, kupigia mfano Qur'ani wa wanawake wawili waumini, yaani Maryam na Asiya (mke wa Firauni), ni kuonyesha kigezo cha kufuatwa na wanaume na wanawake wote waumini na kiashiria cha umuhimu wa fikra na matendo ya wanawake, na akafafanua kwa kusema: haki za kijamii za wanawake, kama vile kulipwa mshahara sawa na wanaume kwa kazi ya aina moja, bima kwa wanawake walioajiriwa au wanaoendesha familia, likizo maalumu kwa wanawake, na masuala mengine mengi, lazima yachungwe na kuzingatiwa bila ubaguzi.

Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria mwenendo wa Magharibi wa kukazania kueneza utamaduni wake potofu duniani na kueleza kwamba: "wao wanadai kuwa mipaka maalumu iliyowekwa kwa ajili ya mwanamke, ikiwemo hijabu, vitazuia maendeleo yake, lakini Jamhuri ya Kiislamu imebatilisha mantiki hii potofu na kuonyesha kwamba wanawake Waislamu walioshikamana na vazi la stara la Kiislamu, wanaweza kusonga mbele na kutoa mchango zaidi katika nyanja zote kuliko wanawake wengine". .../