Pars Today
Mamilioni ya wananchi wa Sudan wameandamana Khartoum mji mkuu wa Sudan kwa mwaliko wa kamati ya uratibu wa mapambano katika maandamano yaliyopewa jina la "Tumechoka".
Mkuu wa Baraza la Uongozi la Sudan amesisitiza kuhusu vikosi vya ulinzi vya nchi hiyo kuachana na shughuli za kisiasa.
Basi ya abiria mapema leo liligonga lori lililokuwa limeegeshwa katika barabara kuu kwenye mji wa Omdurman huko Sudan na kuuwa watu wasiopungua 16.
Mapigano ya kikabila yaliyozuka katika eneo la Darfur nchini Sudan yamesababisha vifo vya saba, huku wengine kadhaa wakijeruhiwa.
Makubaliano ya kusuluhisha mgogoro wa kisiasa wa Sudan yametiwa saini na vyama vya kisiasa vya nchi hiyo katika hali ambayo wengi wana wasiwasi kuhusu mustakabali wa nchi hiyo na uingiliaji wa nchi za kigeni katika mambo ya ndani ya nchi hiyo ya Kiafrika.
Antonio Guterres Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amekaribisha na kuunga mkono kusainiwa makubaliano kati ya makundi ya kiraia ya kisiasa na jeshi la Sudan kwa ajili ya kuupatia ufumbuzi mgogoro wa kisiasa nchini humo.
Maelfu ya wananchi wa Sudan wamefanya maandamano ya kupinga makubaliano ya amani yanayotazamiwa kusainiwa kesho Jumatatu kwa shabaha ya kuhitimisha mgogoro wa kisiasa wa nchi hiyo.
Makundi ya kiraia na utawala wa kijeshi unaongoza hivi sasa nchini Sudan zinatazamiwa kusaini makubaliano ya kisiasa Jumatatu ijayo, kwa shabaha ya kuhitimisha mgogoro wa kisiasa wa nchi hiyo.
Mamlaka za afya nchini Sudan zimetangaza habari ya kuaga dunia makumi ya watu kutokana na mripuko wa homa ya Dengi (Dengue) nchini humo.
Wafuasi wa chama tawala cha zamani nchini Sudan na baadhi ya vyama vya kisiasa wameandamana mjini Khartoum, mji mkuu wa nchi hiyo, kupinga uingiliaji wa madola ya kigeni katika masuala ya ndani ya Sudan.