Mamilioni ya wananchi wa Sudan waandamana dhidi ya serikali ya kijeshi
(last modified Wed, 18 Jan 2023 08:36:41 GMT )
Jan 18, 2023 08:36 UTC

Mamilioni ya wananchi wa Sudan wameandamana Khartoum mji mkuu wa Sudan kwa mwaliko wa kamati ya uratibu wa mapambano katika maandamano yaliyopewa jina la "Tumechoka".

Wakazi wa mji mkuu Khartoum jana alasiri waliandamana kwa wingi katika mitaa mbalimbali ya mji mkuu Khartoum dhidi ya serikali ya kijeshi huku wakipiga nara mbalimbali na kwa mara nyingine tena wamesisitiza kuondoka madarakani wanajeshi na kuundwa serikali ya kiraia na ya kisheria.  

Ahmad Fadhil kijana raia wa Sudan aliyeshiriki maandamano hayo ameliambia shirika la habari la Iran Press huko Khartoum kuwa: ujumbe wa wananchi wa Sudan walioandamana ni huu kuwa, serikali ya kijeshi inapasa kung'olewa madarakani na Wasudani hawafanyi mazungumzo na wanajeshi." 

Zuahir al Bakr mwandamanaji mwingine huko Khartoum amesema kuwa, wananchi wa Sudan hawatafanya mazungumzo na serikali ya kijeshi na wataendelea kuandamana hadi kuhitimishwa serikali ya kijeshi nchini humo. 

Maelfu ya Wasudan katika wiki za karibuni pia wamefanya maandamano katika mji mkuu Khartoum, Omdurman na katika miji mingine kulalamikia mapatano ya karibuni kati ya makundi ya kiraia na jeshi kwa lengo la kupata njia za kutatua mgogoro wa kisiasa nchini humo. 

Maandamano Sudan dhidi ya serikali ya kijeshi 

Mapatano hayo ambayo yanahesabiwa kuwa msingi wa utatuzi wa mgogoro wa kisiasa wa Sudan yalisainiwa huko Khartoum na makundi ya kiraia na baraza la Uongozi wa Mpito la Sudan  kwa kuhudhuriwa na viongozi wa ndani, kikanda na kimataifa.  

Tags