-
UN: Sudan kukumbwa na mgogoro mbaya zaidi wa kibinadamu duniani
Mar 21, 2024 06:42Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imeonya kuwa, mapigano makali ya karibu mwaka mmoja sasa kati ya makundi mawili hasimu, yaani Jeshi la Sudan (SAF) na Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) yameiweka nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika katika ncha ya kutumbukia kwenye mgogoro mbaya zaidi wa njaa duniani.
-
UN yazitaka pande za Sudan kuweka chini silaha, kuwalinda raia wakati wa Ramadhani
Mar 16, 2024 22:41Umoja wa Mataifa umezitaka pande zinazozozana Sudan kuweka chini silaha na kuwalinda raia wakati huu wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.
-
Sudan karibuni itakumbwa na janga kubwa la njaa
Mar 06, 2024 04:12Mpango wa Chakula Duniani (WFP) leo umetahadharisha kuwa vita vya Sudan vilivyodumu kwa takriban miezi 11 kati ya majenerali hasimu vinahatarisha nchi hiyo kuathiriwa na janga kubwa la njaa.
-
Khartoum yakanusha madai kuwa Iran inataka kujenga kambi ya kijeshi Sudan
Mar 04, 2024 07:15Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan amekadhibisha madai ya gazeti moja la Marekani kwamba Iran imeiomba serikali ya Sudan idhini ya kujenga kituo cha kudumu cha kijeshi katika maji ya Bahari Nyekundu, pwani ya nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.
-
Ripoti ya UN: RSF inashambulia na kuua raia Darfur, Sudan kwa msingi wa ukabila
Mar 01, 2024 23:38Ripoti mpya ya wataalamu wa Umoja wa Mataifa imesema, Vikosi vya Usaidizi wa Haraka RSF pamoja na wanamgambo vinaoshirikiana nao wanaopigania kutwaa madaraka nchini Sudan wamefanya mauaji ya kikabila na ubakaji wakati wa udhibiti wa eneo kubwa la Darfur magharibi mwa nchi hiyo, na kwamba vitendo hivyo vinaweza kuwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu.
-
Sudan yapuuzilia mbali madai ya Marekani dhidi yake
Feb 25, 2024 06:26Serikali ya Sudan imekosoa vikali taarifa ya Marekani inayotuhumu serikali ya Khartoum kwamba inazuia watu nchi humo kufikishiwa misaada ya kibinadamu.
-
Kufufuka uhusiano wa Iran na Sudan kwaitia wahka mkubwa Marekani
Feb 25, 2024 02:54John Godfrey, balozi wa Marekani nchini Sudan, amesema katika taarifa ya uingiliaji wa wazi wa mambo yasiyomuhusu ndewe wala sikio kwamba eti ana wasiwasi wa kuimarika uhusiano kati ya Iran na Sudan kwa madai kuwa uhusiano huo utaifanya Iran iisaidie kijeshi Sudan.
-
UN: Makumi ya watu wamebakwa, kunyanyaswa kingono nchini Sudan
Feb 23, 2024 22:44Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema katika ripoti yake mpya iliyotolewa jana Ijumaa kwamba makumi ya watu, wakiwemo watoto, wamekuwa waathiriwa wa ubakaji na aina nyingine za unyanyasaji wa kingono katika mzozo unaoendelea nchini Sudan, vitendo ambavyo vinaweza kutambuliwa kuwa ni uhalifu wa kivita.
-
Le Monde: Hakuna matumaini ya kukomeshwa vita hivi karibuni nchini Sudan
Feb 11, 2024 08:37Ripoti iliyochapishwa na gazeti la Ufaransa la Le Monde imesema kwamba, baada ya zaidi ya miezi 9 ya vita kati ya Jeshi la Sudan linaloongozwa na Abdel Fattah al-Burhan na Vikosi vya Msaada wa Haraka chini ya uongozi wa Mohamed Hamdan Dagalo, hakuna uwezekano wa kumalizika vita hivyo karibuni.
-
Mkurugenzi wa kampuni ya mawasiliano ya simu: RSF imekata mawasiliano kote Sudan
Feb 10, 2024 03:52Afisa wa huduma za mawasiliano wa Sudan amesema Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) ndivyo vinavyohusika na kukatika mawasiliano kote Sudan kwa siku ya nne mfululizo.