Pars Today
Viongozi wa Sudan wamechukua uamuzi wa kukifunga kivuko cha mpakani kati ya nchi hiyo na Ethiopia.
Serikali ya Sudan ili iondolewe katika orodha ya Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Marekani ya mataifa eti yanayounga mkono ugaidi, imeilipa Washington fidia ya mamilioni ya dola katika tukio la kushambuliwa balozi za Marekani huko Tanzania na Kenya.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani amesema kuwa, serikali ya Sudan imeilipa fidia nchi hiyo kutokana na mashambulizi ya mabomu ya mwaka 1998 kwenye balozi za Marekani za Nairobi na Dar es Salaam katika nchi za Kenya na Tanzania.
Maafisa watano wa serikali ya Sudan wamekufa maji baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kuzama kutokana na hali mbaya ya hewa kaskazini mwa nchi hiyo.
Mkuu wa Baraza la Uongozi la utawala wa mpito Sudan amesema kuwa nchi yake imejiandaa kwa lolote na kuitaka Ethiopia kujiweka mbali na ardhi ya Sudan.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia amedai kuwa, sehemu kubwa ya akiba ya maji ya Mto Nile ni mali ya nchi yake.
Sudan imeituhumu serikali ya Ethiopia kuwa inalipatia silaha kundi moja la uasi ili kuudhibiti mji wa al Karmak huko kusini mashariki mwa Sudan.
Waziri wa Umwagiliaji na Vyanzo vya Maji wa Sudan amesema kuwa, nchi yake inakusudia kuandaa uungaji mkono na upatanishi wa pande nne kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi mzozo wa Bwawa la al-Nahdha.
Duru za kuaminika nchini Sudan zimeripoti kuwa, mjumbe wa Umoja wa Afrika alitazamiwa kuwasili Khartoum akiongoza ujumbe wa upatanishi wa umoja huo katika mzozo wa mpakani baina ya Sudan na Ethiopia.
Baada ya kupita miaka miwili tokea uanze mgogoro wa Sudan ambao ulipelekea kuondolewa madarakani Rais Omar Al Bashir mnamo Apirli 2019, nchi hiyo ingali inaendelea kushuhudia migogoro kadhaa ya kisiasa, kichumi na kiusalama.