Kivuko cha mpakani kati ya Sudan na Ethiopia chafungwa
Viongozi wa Sudan wamechukua uamuzi wa kukifunga kivuko cha mpakani kati ya nchi hiyo na Ethiopia.
Viongozi wa Sudan wametangaza kuwa, wameamua kukifunga kivuko hicho cha mpakani kati ya nchi hiyo na Ethiopia baada ya kujiri mapigano kati ya vikosi vya jeshi la nchi hiyo na kundi moja la wanajeshi wa Sudan. Watu kadhaa wamejeruhiwa katika mapigano hayo.
Hii ni katika hali ambayo viongozi wa Ethiopia kwa upande wao wamelalamikia uamuzi huo wa Sudan wa kukifunga kivuko hicho cha mpakani na kusisitiza ulazima wa kupatiwa ufumbuzi hitilafu zilizopo na masuala ya kiusalama kati ya pande mbili hizo kupitia mazungumzo.
Viongozi wa Ethiopia wamesisitiza kuwa, kitendo cha kuifunga mipaka chini ya kivuli cha kubadilisha biashara na maslahi ya pamoja kati ya nchi mbili si njia ya kutatua mgogoro.
Wanajeshi wa Sudan hivi karibuni walipigana kwa mara kadhaa na wenzao wa Ethiopia; huku kila upande ukishambulia maeneo ya upande wa pili.
Sudan na Ethiopia zinahitilafiana kuhusu eneo la ardhi ya kilimo huko al Fashaga linalopatikana katika mpaka wa kimataifa wa Sudan; eneo ambalo wakulimwa wa Kiethiopoa wanaishi hapo kwa muda sasa.
Wakati huo huo Khartoum inalituhumu jeshi la Ethiopia kuwa linauwanga mkono wanamgambo wa Kiethiopia.