-
Tuhuma mpya dhidi ya Omar al Bashir zaanza kufuatiliwa nchini Sudan
Jun 10, 2020 21:56Mkuu wa Kamati ya Kupambana na Ufisadi ambaye pia ni mjumbe wa Baraza la Uongozi la Sudan ametangaza habari ya kuanza kufuatiliwa tuhuma mpya zinazomkabilia rais wa zamani wa nchi hiyo, Jenerali Omar Hassan Ahmad al Bashir.
-
Mahakama ya Kimataifa ya Jinai yamkamata kiongozi wa Janjaweed
Jun 10, 2020 00:54Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) imetangaza kuwa, kiongozi wa wanamgambo wa Janjaweed Ali Kosheib ambaye alikuwa mtu wa karibu kwa rais wa zamani wa Sudan, Omar al Bashir amejisalimisha kwa mahakama hiyo na kwamba anakabiliwa na tuhuma za kutenda jinai za kivita katika jimbo la Darfur huko magharibi mwa Sudan tangu mwaka 2003.
-
Ethiopia yaituhumu Misri kuwa imechochea ghasia na machafuko nchini humo
Jun 04, 2020 07:13Afisa wa serikali ya jimbo la Oromia nchini Ethiopia ameituhumu serikali ya Misri kuwa imechochea maandamano na ghasia zilizoshuhudiwa katika siku za hivi karibuni jimboni humo.
-
Ethiopia yatilia mkazo mashauriano ya kidiplomasia ili kutatua hitilafu kati yake na Sudan
May 31, 2020 23:27Wizara ya Mambo ya Nje ya Ethiopia imetoa taarifa na kusisitiza kufanyika mashauriano ya kidiplomasia ili kuzipatia ufumbuzi hitilafu baina yake na Sudan.
-
Siri ya kutua ndege ya utawala haramu wa Kizayuni kwenye ardhi ya Sudan, yafichuka
May 28, 2020 21:53Ndege ya utawala haramu wa Israel ambayo hivi karibu ilitua katika ardhi ya Sudan, ilikuwa na lengo la kumuokoa dalali anayefuatilia kuboreshwa uhusiano wa nchi hiyo na Tel Aviv ambaye alikuwa ameambikizwa virusi vya Corona.
-
Wakati Saudia na Imarati zinapoitumia vibaya Sudan na baadaye kuiacha "solemba"
May 26, 2020 02:19Kwa muda sasa Sudan imebadilisha misimamo yake ya kisiasa kama njia ya kuvutia misaada ya kifedha kutoka kwa nchi kama Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) na Saudi Arabia lakini nchi hizo hazioneshi utashi wowote wa kuitatulia Khartoum matatizo yake zaidi ya kuitumia tu kufanikishia malengo yao binafsi.
-
Sudan yakaribia "kumezwa" na utawala wa Kizayuni wa Israel
May 24, 2020 23:26Katika hatua nyingine ya kushangaza na ambayo inaashiria jinsi Israel ilivyo na hamu ya kuimeza nchi ya Waislamu ya Sudan, Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni amezungumza kwa simu na mkuu wa Baraza la Uongozi la Sudan na kuitaka Khartoum ijikurubishe zaidi na zaidi kwa utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Sudan: Tumeondoa akthari ya askari wetu nchini Yemen
May 15, 2020 07:55Serikali ya Mpito wa Sudan imetangaza kuwa imewaondoa nchini Yemen aghalabu ya wanajeshi wake waliokuwa wanapigana chini ya muungano vamizi wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia.
-
Watu 26 wauawa katika mapigano ya kikabila kusini mwa Sudan
May 14, 2020 06:34Watu wasiopungua 26 wanaripotiwa kuuawa kusini mwa Sudan na wengine 19 kujeruhiwa baada ya kuibuka mapigano ya kikabila katika jimbo la Kordofan Kusini.
-
Mapigano ya kikabila Darfur, Sudan yaua watu 30
May 07, 2020 03:28Kwa akali watu 30 wameuawa huku wengine wengi wakijeruhiwa katika mapigano ya kikabila baina ya Waarabu na wasiokuwa Waarabu katika mkoa wa Darfur Magharibi nchini Sudan.