Kiongozi wa Baraza la Uongozi la Sudan afichua njama ya kutaka kumuuwa
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i62481-kiongozi_wa_baraza_la_uongozi_la_sudan_afichua_njama_ya_kutaka_kumuuwa
Naibu Mkuu wa Baraza la Uongozi la Sudan ametangaza kuwa panden kadhaa nchini humo zimetishia kumuuwa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 28, 2020 22:31 UTC
  • Kiongozi wa Baraza la Uongozi la Sudan afichua njama ya kutaka kumuuwa

Naibu Mkuu wa Baraza la Uongozi la Sudan ametangaza kuwa panden kadhaa nchini humo zimetishia kumuuwa.

Mohamed Hamdan Dagalo ameyatahadharisha makundi hayo yaliyotishia kutekeleza mauaji dhidi yake. Naibu Mkuu wa Baraza la Uongozi la Sudan ameyatuhumu makundi hayo kwa kujaribu kuvuruga na kubomoa nchi, kuvuruga muundo wa kjamii na kusambaratisha umoja wa Sudan na kusema kuwa atakabiliana na pande hizo kwa gharama yoyote ile.  

Dagalo ameonya kuhusu njama za kutaka kuigawa Sudan, magenge ya magendo ya dhahabu  na kuyatahadharisha makundi yanayojaribu kuzima mchakato wa kiuchumi wa nchi hiyo. 

Mohamed Hamdan Dagalo amewakosoa wale wote wanaopinga yeye kuwa kusimamia Kamati ya Kiuchumi iliyoundwa mwezi Machi mwaka huu.  

Sudan ilikumbwa na maandamano ya wananchi dhidi ya serikali ya Rais wa wakati huo wa Sudan Omar Hassan al bashir tangu mwezi Disemba mwaka juzi; na  kupelekea kung'olewa madarakani rais huyo mwezi Aprili mwaka jana. Aidha baada ya kupita miezi kadhaa ya machafuko ya kisasa na maandamano ya wananchi; Baraza la Kijeshi la Uongozi Sudan lilikabidhi madaraka ya nchi kwa serikali ya mpito ya hivi sasa.  

Omar Hassan al Bashir, Rais wa Sudan aliyepinduliwa madarakani