-
Rais wa Tanzania: Shule zote zifunguliwe Juni 29, aruhusu harusi
Jun 16, 2020 12:24RAIS wa Tanzania, John Pombe Magufuli ameagiza shule zote nchini humo zifunguliwe tarehe 29 Juni 2020 baada ya kuwepo kwa mwenendo mzuri wa maambukizi machache ya ugonjwa wa Corona.
-
SAUTI, Mufti wa Tanzania Abubakar Zubeir atoa mwongozo kuhusu Corona, Waislamu Kenya walaani mauaji ya polisi wa nchi hiyo dhidi ya baba na watoto wake wawili
Jun 05, 2020 16:05Ripoti ya matukio ya Kiislamu inahusu mwongozo uliotolewa na Mufti wa Tanzanua Sheikh Abubakar Zubeir Ali leo Ijumaa kuhusiana na ugonjwa wa Corona ambapo amemshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kuitikia Dua za watanzania.
-
Tanzania yamuita Kaimu Balozi wa Marekani ajieleze kuhusu taarifa za corona
May 27, 2020 08:04Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ya Tanzania imemuita Kaimu Balozi wa Marekani nchini humo, Dakta Imni Patterson atoe ufafanuzi kuhusu taarifa ambazo amekuwa akiziandika kwenye mitandao yake ya kijamii bila uthibitisho.
-
Waziri wa Afya wa Tanzania: Mashine moja ya kupima Corona ilikuwa na matatizo
May 23, 2020 15:44Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wa Tanzania Ummy Mwalimu ametoa taarifa kuhusu uchunguzi uliofanywa kuilenga maabara ya taifa ambapo ameeleza mambo kadhaa yaliyogunduliwa na kamati teule ya uchunguzi huo.
-
Tanzania yafungua anga na kuruhusu ndege kuendelea kuingia na kutoka nchi hiyo
May 18, 2020 15:37Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetangaza rasmi kufungua anga yake na kuruhusu ndege zote kuendelea kutua au kupita katika anga ya nchi hiyo baada ya kufungwa kuanzia tarehe 7 Mei mwaka huu katika jitihada za kukabiliana na kuenea kwa virusi vya Corona.
-
Wabunge wa CHADEMA waliojitenga na watu kwa sababu ya Corona wamerejea leo bungeni
May 15, 2020 14:59Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA nchini Tanzania kimetoa taarifa kikisema kuwa, wabunge wote wa Chama hicho ambao hatimae wamehitimisha siku 14 za kujiweka karantini kwa kukaa nyumbani na kutohudhuria shughuli za bunge, pamoja na vikao vya bunge au kufika ndani ya ukumbi na kamati zake katika maeneo mengine ya mhimili huo, leo Ijumaa, wamerejea bungeni kuendelea na majukumu yao, baada ya kuwa na uhakika kuwa hawana maambukizi ya Ugonjwa wa COVID19, unaosababishwa na virusi vya Corona.
-
Rais Magufuli awataka Watanzania wachape kazi licha ya maambukizi ya corona
May 03, 2020 11:20Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania amewataka wananchi wa nchi hiyo wasiwe na hofu yoyote ya corona na waendelee kuchapa kazi kama kawaida.
-
Vifo vya Corona nchini Tanzania vyafikia 16, maabukizi yakaribia 500
Apr 29, 2020 11:28Idadi ya watu walioaga dunia kwa ugonjwa wa Covid-19 (Corona) nchini Tanzania imeongezeka na kufikia watu 16.
-
Kampeni za uchaguzi mkuu kuanza kesho Jumatatu nchini Burundi
Apr 26, 2020 11:35Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi ametia saini rasmi amri ya kuanza kampeni za uchaguzi mkuu wa rais bunge na madiwani nchini humo. Kampeni hizo zitaanza kesho Jumatatu na kuendelea hadi Jumapili ya tarehe 17 mwezi ujao wa Mei.
-
Baada ya kuongezeka wagonjwa 23, idadi ya walioambukizwa virusi vya corona Zanzibar yafikia 58
Apr 19, 2020 15:01Wizara ya Afya ya Zanzibar imetangaza wagonjwa wapya 23 wa Homa Kali ya Mapafu inayosababishwa na virusi vya corona vya COVID-19.