-
Bernard Membe: Kamati Kuu ya CCM ilifanya uamuzi wa haraka dhidi yangu na kuwaaminisha Watanzania ndivyo sivyo
Mar 09, 2020 11:28Aliyekuwa kada wa chama tawala nchini Tanzania CCM na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Bernard Membe, amesema kuwa kamati kuu ya chama hicho ilifanya haraka kutangaza mapendekezo yake ya kumfukuza ndani ya chama kabla ya kuchukuliwa uamuzi.
-
Dk Bashiru amjibu Membe, asema kama tatizo ni urais tukutane uwanjani
Mar 02, 2020 09:45Katibu Mkuu wa chama cha Mapinduzi CCM nchini Tanzania, Dk Bashiru Ally amemjibu Bernard Membe aliyekuwa kada wa chama hicho na Waziri wa Mambo ya Nje wa Zamani wa nchi hiyo, akimtaka kugombea urais kwa tiketi ya chama kingine cha siasa ili wakutane uwanjani.
-
Watanzania waendelea kutoa radiamali kufuatia Bernard Membe kupigwa kalamu nyekundu na CCM
Mar 01, 2020 11:19Uamuzi wa Kamati Kuu ya chama cha Mapinduzi CCM wa kumfukuza uanachama Bernard Membe kada wa chama hicho na aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, umepokelewa kwa hisia tofauti na Watanzania.
-
Tanzania: Uchaguzi wa mwaka huu utakuwa huru na wa haki, hatukiuki haki za binaadamu ni propaganda tu
Feb 27, 2020 12:59Serikali ya Tanzania kupitia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi imeihakikishia dunia kwamba uchaguzi mkuu ujao, utakuwa huru na wa haki.
-
Hatimaye Erick Kabendera aachiliwa huru baada ya kukiri makosa na kulipa sehemu ya faini
Feb 24, 2020 10:29Hatimaye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya jijini Dar es salaam imemwachilia huru mwandishi wa habari za uchunguzi, Erick Kabendera na kumwamuru alipe faini na fidia ya jumla ya Shilingi milioni 273 baada ya kukiri makosa yaliyokuwa yanamkabili yakiwemo ya utakatishaji fedha na ukwepaji kodi huku akiondolewa shitaka la kuongoza genge la uhalifu.
-
Kambi ya upinzani Tanzania yapata pigo jingine baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema kutimkia CCM
Feb 18, 2020 13:12Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama kikuu cha upinzani cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) nchini Tanzania Dk Vicent Mashinji leo Jumanne Februari 18 amehamia chama tawala CCM na kupokewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Humphrey Polepole.
-
Balozi Kairuki: Serikali Haitawarudisha Tanzania wanafunzi walioko China + Sauti
Feb 12, 2020 09:20Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki amesema wanafunzi wanaosoma katika mji wa Wuhan hawawezi kurudi kwa sababu kuna katazo la kutoingia wala kutoka kwenye mji huo kutokana na maambukizi ya virusi vya corona.
-
Rais wa Tanzania amfuta kazi afisa wa serikali aliyeichana Qurani
Feb 11, 2020 09:24Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli amemuagiza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo, kuhakikisha anamuandikia barua ya kumfukuza kazi mfanyakazi wa wizara hiyo aliyechana na kuitemea mate Qurani Takatifu mkoani Morogoro.
-
Membe: Nimefurahi sana kuhojiwa na Kamati ya CCM, sehemu ya niliyoulizwa itakuwa ikitoka kidogokidogo
Feb 06, 2020 12:42Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje nchini Tanzania, Bernard Membe amesema kuwa safari yake ya kwenda Dodoma ilikuwa ya manufaa makubwa sana kwake, kwa chama cha Mapinduzi CCM na kwa Taifa na kwamba masuala mengine aliyohojiwa na kamati ya chama hicho yataendelea kutoka kidogokidogo hapo baadaye.
-
Wanajeshi 10 wa Tanzania wapoteza maisha wakati wakifanya mazoezi
Feb 03, 2020 10:39Jeshi la Ulinzi la Tanzania limetangaza kuwa askari 10 wa jeshi hilo wamepoteza maisha wakati wakifanya mazoezi.