-
Radiamali za nchi zilizowekewa vikwazo vya usafiri na Marekani
Feb 02, 2020 04:04Serikali ya Eritrea imekosoa vikali hatua ya Washington ya kuwawekea vizingiti raia wa nchi hiyo ya Pembe ya Afrika wanaotaka kwenda Marekani ikisisitiza kuwa, vikwazo hivyo vya usafiri havikubaliki.
-
Makumi wapoteza maisha wakigombania 'mafuta ya upako' Tanzania + Sauti
Feb 02, 2020 00:13Kwa akali watu 20 wameaga dunia katika mkanyagano wa harakati za kutaka kukanyaga 'mafuta ya upako' kwenye kongamano la 'Mtume' Boniface Mwaiposa lililofanyika uwanja wa Majengo mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, kaskazini mashariki mwa Tanzania jioni ya jana Jumamosi.
-
Baada ya Lugola kupigwa kalamu nyekundu, Rais Magufuli amemteua Simbachawene kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania
Jan 23, 2020 12:30Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania amemteua George Simbachawene kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Kangi Lugola mbunge wa Mwibara (CCM). Hayo yameelezwa jioni ya leo na katibu mkuu kiongozi, Balozi John Kijazi.
-
Tanzania, Nigeria katika nchi zitakazowekewa vikwazo vya usafiri na Marekani
Jan 22, 2020 08:37Marekani ina mpango wa kuziongeza nchi nyingine saba zikiwemo Tanzania na Nigeria kwenye orodha ya nchi ambazo raia wake wanatarajiwa kuwekewa vikwazo na vizingiti vya kuingia nchini humo.
-
Magufuli awaambia polisi: Wakamateni wale wote wanaovihusisha vyombo vya usalama na matukio ya kupotea watu
Jan 13, 2020 04:47Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania amelitaka jeshi la polisi kuwakamata na kuwachukulia hatua kali za kisheria watu wanaovihusisha vyombo vya ulinzi na usalama ikiwamo Idara ya Usalama wa Taifa (Tiss), na matukio ya kupotea na kutekwa nyara watu.
-
Wazanzibar: Miaka 56 baadaye, malengo ya Mapinduzi hayajafikiwa
Jan 12, 2020 13:14Sherehe za maadhimisho ya miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar zimefanyika leo Jumapili katika Uwanja wa Abeid Aman Karume kisiwani Unguja.
-
Mkuu wa Mkoa wa Tabora afuta mapumziko ya Mwaka Mpya; watu wakalime pamba + Sauti
Dec 15, 2019 12:50Nchini Tanzania, Mkuu wa mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri, ameagiza kuakhirishwa likizo ya A-Mass na mwaka mpya kwa maafisa wa kilimo na maafisa wote katika kipindi hiki cha mvua, ili watoke waende vijijini wakawahimize wananchi kulima pamba kwa ubora unaotakiwa. Ammar Dachi na maelezo zaidi kutoka Dar es Salaam, Tanzania
-
SAUTI, Usikose kutegea sikio ripoti ya matukio ya Kiislamu, kuanzia Tanzania hadi nchini Kenya
Dec 13, 2019 13:09Ripoti hii ya matukio ya Kiislamu imesheheni habari za Ijtimai iliyofanyika visiwani Zanzibar, ukaguzi wa msikiti mkubwa zaidi eneo la jangwa la sahara unaojengwa na Mfalme wa Sita wa Morocco nchini Tanzania, safari ya Mufti wa Tanzania Abubakar Zuberi nchini Morocco kuhudhuria kongamano la Kiislamu na hadi mjini Nyeri nchini Kenya.
-
Wanyamapori waua watu 96 nchini Tanzania
Dec 09, 2019 04:38Watu zaidi ya 96 wameuawa na wengine 90 wamejeruhiwa kutokana na wanyamapori waliovamia mashamba na maeneo ya makazi nchini Tanzania tangu Julai mwaka 2018 hadi Julai mwaka 2019.
-
Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania ajitoa Chadema + Video
Dec 04, 2019 08:14Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania, Frederick Tluway Sumaye ameng'oka rasmi kwenye chama cha upinzani cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA.