Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania ajitoa Chadema + Video
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i57671-waziri_mkuu_wa_zamani_wa_tanzania_ajitoa_chadema_video
Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania, Frederick Tluway Sumaye ameng'oka rasmi kwenye chama cha upinzani cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
Dec 04, 2019 08:14 UTC
  • Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania ajitoa Chadema + Video

Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania, Frederick Tluway Sumaye ameng'oka rasmi kwenye chama cha upinzani cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA.

Akizungumza na waandishi wa habari, Sumaye amesema kuwa kuanzia leo Jumatano tarehe 4 Disemba, 2019 yeye si mwanachama tena wa Chadema.

Sumaye aliitisha mkutano huo jana Jumanne Desemba 3, 2019 na kuahidi kuzungumzia masuala ya kisiasa na uchaguzi wa Chadema unaoendelea.

Kuliibuka hisia tofauti baada ya tangazo hilo la Sumaye huku watu wengi wakitabiri kuwa angelichukua hatua kali kutokana na hali iliyojitokeza kwenye uchaguzi wa ndani ya chama chake.

Sumaye alikuwa Waziri Mkuu wa Tanzania kuanzia mwaka 1995 hadi 2005.

Alishindwa kupata kura katika uchaguzi wa mwenyekiti wa DHADEMA Kanda ya Pwani kwa kuoigiwa kura 48 za hapana kati ya 76. Hata hivyo, taratibu za chama cha CHADEMA zinasema kuwa, uchaguzi huo itabidi urudiwe.

Vile vile amesema, katika uchaguzi huo wajumbe wa mkutano walishawishiwa na baadhi ya viongozi walioshiriki kumchukulia fomu za kuwania uenyekiti ili asishinde.

Amesema: "Nimelazimika kwa kulazimishwa kujiondoa Chadema na kuanzia sasa si mwana Chadema na sijiungi na chama chochote cha siasa. Nitakuwa tayari kutumika na chama chochote ikiwamo Chadema.”