-
Guterres apuuza mashinikizo ya US ya kutaka asusie Olimpiki China
Feb 03, 2022 09:12Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amepuuzilia mbali mwito wa Balozi wa Marekani katika umoja huo wa kumtaka asusie hafla ya ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya msimu wa baridi kali nchini China.
-
UN yaitaka jamii ya kimataifa izidi kulishinikiza jeshi Myanmar likomeshe ukatili
Jan 29, 2022 04:35Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet ameitaka jamii ya kimataifa izidishe mashinikizo kwa jeshi la Myanmar ili likomeshe kampeni yake ya ukatili na ukandamizaji dhidi ya watu wa Myanmar na kusisitiza kurejeshwa mara moja utawala wa kiraia nchini humo.
-
UN yalaani mashambulizi ya Saudia dhidi ya jela ya Yemen, makumi ya mahabusu wameuawa
Jan 22, 2022 04:38Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelaani mashambulizi ya ndege za kivita za Saudi Arabia dhidi ya jela ya wafungwa katika mkoa wa Sa'ada nchini Yemen.
-
Umoja wa Mataifa: Kunahitajika dola bilioni 3.9 kwa ajili ya kuwasaidia Wayamen
Jan 13, 2022 08:07Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika uratibu wa masuala ya kibinadamu (OCHA) ametangaza kuwa, kunahitajika dola bilioni 3.9 kwa ajili ya kuwasaidia mamilioni ya wananchi wa Yemn wanaohitahia misaada ya kibinadamu.
-
Wataalamu wa UN waitaka Marekani ifunge gereza la Guantamano
Jan 11, 2022 04:19Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wameutaka utawala wa Rais Joe Biden wa Marekani utekeleze ahadi yake ya kufunga jela ya kutisha ya Guantanamo Bay iliyoko nchini Cuba.
-
UN yasitisha misaada ya kibinadamu katika eneo la Tigray, Ethiopia
Jan 10, 2022 03:10Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa umesitisha operesheni za kupeleka misaada ya kibinadamu katika jimbo la Tigray baada ya ndege za kijeshi za Ethiopia kushambulia kambi ya wakimbizi katika eneo hilo.
-
Wanataaluma wa Sudan wapinga mazungumzo ya UN
Jan 09, 2022 09:57Chama cha Wanataaluma cha Sudan ambacho kiliongoza maandamano ya wananchi yaliyopelekea kung'olewa madarakani utawala wa aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Omar al Bashir, kimetangaza kuwa hakiungi mkono mazungumzo yaliyoitishwa na Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kujaribu kuupatia ufumbuzi mgogoro wa kisiasa nchini humo.
-
Umoja wa Mataifa waunga mkono kufanyika uchaguzi wa Libya katika wakati mwafaka
Dec 24, 2021 08:08Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amehimiza kufanyika uchaguzi mkuu wa Bunge na Rais katika tarehe mwafaka nchini Libya.
-
UN yaiongezea MONUSCO muda wa kuhudumu nchini Kongo DR
Dec 21, 2021 23:13Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeuongezea muda wa mwaka mmoja Ujumbe wake wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo MONUSCO na kuwataka walinda amani wa ujumbe huo kuelekeza nguvu zao Kaskazini-Mashariki mwa nchi, huku likisisitizia kufanyika operesheni za pamoja na vikosi vya nchi hiyo, FARDC.
-
Umoja wa Mataifa wawataka viongozi wa Lebanon kutanguliza mbele matakwa vya wananchi
Dec 20, 2021 04:20Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amewataka viongozi wa Lebanon kufanya kazi kwa pamoja ili kutatua migogoro iliyopo nchini humo, huku akitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuisaidia na kuiunga mkono Lebanon kutokana na matatizo yake ya sasa.