-
Safari ya Grossi nchini Iran na kuwekwa wazi maendeleo ya amani ya nishati ya nyuklia ya Iran
May 07, 2024 04:47Rafael Grossi, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA aliwasili mjini Tehran Jumatatu akiongoza ujumbe alioandamana nao kwa ajili ya kushiriki katika mkutano wa kimataifa wa nyuklia na vilevile kufanya mazungumzo na viongozi wakuu wa nyuklia na kisiasa wa nchini.
-
Maseneta 12 wa Marekani waitishia ICC: Mkiiandama Israel tutakuandameni
May 07, 2024 03:08Maseneta 12 wa chama cha Republican nchini Marekani wameitishia Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) kwamba itawekewa vikwazo na Washington endapo itatoa hati za kukamatwa viongozi wakuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel kwa tuhuma za kuhusika na jinai za kivita katika Ukanda wa Ghaza.
-
Borrell: EU na Jamii ya Kimataifa zinapaswa kuzuia uvamizi na mashambulio ya Israel Rafah
May 07, 2024 03:06Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya amesema, amri iliyotolewa na utawala wa Kizayuni wa Israel ya kuwataka wakazi wa mashariki ya Rafah kusini mwa Ukanda wa Ghaza wahame katika eneo hilo haikubaliki.
-
Vyombo vya habari Iraq vimekatazwa kutumia jina 'Israel', vinauita 'Utawala wa Kizayuni'
May 05, 2024 23:01Vyombo vya habari vya Iraq vimeacha kutumia neno "Israel" kumaanisha utawala wa Tel Aviv na badala yake vinatumia msamiati "Utawala wa Kizayuni" katika hatua ya kuonyesha mshikamano na Wapalestina kwa miezi kadhaa sasa.
-
Afisa wa kijeshi wa Israel: Kuivamia Rafah si hakikisho la kuwakomboa mateka
May 03, 2024 23:02Afisa wa zamani wa wizara ya vita ya utawala wa Kizayuni wa Israel amesema, uvamizi wa jeshi la utawala huo katika mji wa Rafah si hakikisho la kukombolewa na kurejeshwa mateka wake wanaoshikiliwa na makundi ya Wapalestina.
-
Kashfa ya kutoweka raia 10,000 wa Palestina katika vita vya Gaza
May 03, 2024 23:00Sambamba na kuendelea kupanuka maandamano ya wanafunzi wa Marekani na juhudi za Mahakama ya ICJ na ICC za kutoa waranti wa kukamatwa viongozi wa utawala wa kibaguzi wa Israel kutokana na jinai zao huko Gaza, Shirika la Haki za Binadamu la Euro-Mediterranean limetoa ripoti mpya na ya kutisha inayoweza kuzidisha hasira za wanafunzi hao na wakati huo huo kuongeza ushahidi mpya katika jinai zinazofanywa na utawala huo dhidi ya Wapalestina.
-
Kuongezeka ukatili dhidi ya wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Marekani wanaounga mkono Palestina
May 03, 2024 07:14Huku maandamano ya wanafunzi wa vyuo vikuu vya Marekani yakiendelea kufanyika kwa lengo la kupinga jinai za utawala wa Kizayuni huko Gaza na vilevile kwa ajili ya kuwaunga mkono Wapalestina, polisi wa nchi hiyo wameongeza hatua zao za ukandamizaji dhidi ya wanafunzi hao.
-
Ansarullah ya Yemen: Mauaji ya kimbari imekuwa tabia ya kila siku ya Wazayuni
May 03, 2024 04:17Katibu Mkuu wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen ameichukulia mienendo ya kila siku ya utawala wa Kizayuni wa Israel kuwa ni mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Gaza.
-
Kukatwa kikamilifu uhusiano wa Colombia na utawala wa Kizayuni; kuendelea kutengwa Tel Aviv kimataifa
May 02, 2024 23:13Rais Gustavo Petro wa Colombia alisema siku ya Jumatano tarehe Mosi Mei katika hotuba yake kwa mnasaba wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) kuwa kuanzia Alhamisi amekata kikamilifu uhusiano wa nchi hiyo na utawala wa Kizayuni kwa sababu ya jinai na mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala huo huko Ukanda wa Gaza.
-
Iravani: Madai ya uwongo ya Israel dhidi ya Iran; juhudi za kuupotosha ulimwengu kuhusu jinai za Gaza
May 02, 2024 04:13Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa ameyataja madai ya uwongo ya Israel dhidi ya Iran kuwa ni juhudi zenye lengo la kupotosha mazingatio ya walimwengu kuhusu jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya watu wa Ukanda wa Gaza.