-
Kupanuka mpasuko ndani ya serikali ya Israel; Netanyahu kwenye ncha ya wembe
Jan 31, 2024 08:42Moja ya sababu za kushindwa Israel kufikia malengo yaliyokusudiwa katika vita vya Gaza ni kupanuka hitilafu katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu.
-
UN: 'Hakuna mbadala' wa kazi ya UNRWA ya kuokoa maisha ya Wapalestina Gaza
Jan 31, 2024 03:35Mratibu Mwandamizi wa Masuala ya Kibinadamu na Ujenzi mpya wa Gaza Sigrid Kaag amesema, hakuna shirika linaloweza kuchukua nafasi ya shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA, katika Ukanda wa Gaza ulioharibiwa na vita.
-
Sababu za Israel kupenda vita vienee eneo zima la Asia Magharibi
Jan 29, 2024 23:14Duru mbalimbali za habari zimeripoti kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel unafanya njama za kila namna za kutaka vita vienee kwenye eneo zima la Asia Magharibi.
-
Wayemeni waunga mkono mashambulizi dhidi ya meli zinazoelekea Israel
Jan 28, 2024 04:14Kwa mara nyingine tena mamilioni ya wananchi wa Yemen wamefanya maandamano makubwa na kutangaza uungaji mkono wao kwa wananchi wanaodhulumiwa wa Ukanda wa Gaza na vilevile hatua za kijeshi dhidi ya meli inazoelekea ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina.
-
Kan'ani: Msingi wa Israel umejengwa kwa kutegemea mabavu na ubaguzi
Jan 27, 2024 08:55Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa jibu la kiuhasama lililotolewa na utawala wa Kizayuni wa Israel mkabala wa hukumu ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) linaonyesha namna msingi wa utawala huo ulivyojengwa kwa kutegemea vitendo vya mabavu na ubaguzi; na wakati huo huo unadhihirisha namna utawala huo usivyoheshimu kanuni na sheria za kimataifa.
-
Hukumu ya Mahakama ya The Hague; Nukta muhimu katika kutafuta haki kwa ajili ya watu wa Palestina
Jan 27, 2024 08:40Mahakama ya Kimataifa ya Haki, ICJ, yenye makao yake huko The Hague Uholanzi imetoa hukumu yake ya awali kwa shauri la mashtaka lililowasilishwa na Afrika Kusini dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel kuhusu mauaji ya kimbari ya utawala huo huko Ukanda wa Gaza.
-
Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran: Utawala haramu wa Israel umeshindwa kufikia malengo yake Gaza
Jan 26, 2024 08:41Imamu wa muda wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran amesema: Utawala wa Kizayuni umeshindwa katika Ukanda wa Gaza na kwamba, haujafikia lengo lolote kati ya malengo yake.
-
Iran yasisitiza kuwa utawala wa Kizayuni lazima usitishe mauaji ya kimbari Gaza
Jan 26, 2024 04:32Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameisitiza juu ya kusitishwa mauaji ya kimbari yanayotekelezwa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.
-
Hatua mpya za kivita na kichokozi za nchi zaMagharibi katika eneo la Asia Magharibi
Jan 24, 2024 23:25Marekani ikiwa ni mshirika wa kistratijia wa utawala wa Kizayuni wa Israel, ili kudumisha usalama, maslahi ya kiuchumi na kibiashara ya utawala huo katika Bahari Nyekundu, katikati ya mwezi wa Disemba mwaka jana, ilitangaza kuundwa muungano wa baharini lakini muungano huo haukuungwa mkono na nchi za Ulaya isipokuwa Uingereza.
-
Kiongozi Muadhamu: Kuna udharura wa kukatwa mishipa ya uhai ya utawala wa Kizayuni
Jan 23, 2024 10:01Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa: Nchi za Kiislamu zinapaswa kukata uhusiano wao wa kisiasa na kiuchumi na utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kukata mishipa muhimu ya uhai ya utawala huo ghasibu.