Iran yasisitiza kuwa utawala wa Kizayuni lazima usitishe mauaji ya kimbari Gaza
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i107650-iran_yasisitiza_kuwa_utawala_wa_kizayuni_lazima_usitishe_mauaji_ya_kimbari_gaza
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameisitiza juu ya kusitishwa mauaji ya kimbari yanayotekelezwa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.
(last modified 2024-01-26T04:32:26+00:00 )
Jan 26, 2024 04:32 UTC
  • Iran yasisitiza kuwa utawala wa Kizayuni lazima usitishe mauaji ya kimbari Gaza

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameisitiza juu ya kusitishwa mauaji ya kimbari yanayotekelezwa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.

Hossein Amir-Abdollahian, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika mahojiano na Shirika la Habari la ABC mjini New York, Marekani amesisitiza juu ya ulazima wa kusitishwa mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Gaza na ulazima wa kuhakikisha usalama wa Bahari ya Nyekundu (Sham).

Ameongeza kuwa: Wananchi wa Yemen. wanaamini kwamba wanazingatia usalama wa usafiri baharini; Lakini katika uungaji mkono wa Wapalestina wameamua kusimamisha meli zinazoelekea katika bandari zinazokaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni wa Israel ambazo zinapita katika maji ya Bahari Nyekundu, jambo ambalo ni uamuzi wa kijasiri.

 Amir-Abdollahian amekosoa misaada ya silaha ya Marekani kwa utawala wa Kizayuni katika mauaji ya watu wasio na hatia huko Ghaza. Aidha ameashiria juhudi za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran za kurejesha utulivu na amani katika eneo la Asia Magharibi na kubainisha: Kwa njia hiyo Iran ilipigana na Kundi la kigaidi la Daesh/ISIS kwa miaka mingi huko Iraq na Syria, na washauri bora wa kijeshi wa Iran waliuawa shahidi na magaidi katika nchi hizi.

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran amesema mzizi wa migogoro ya Palestina ni zaidi ya miongo saba ya kukaliwa kwa mabavu ardhi hiyo na utawala wa Kizayuni wa Israel. Ameongeza kuwa, kwa mtazamo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) ni harakati ya ukombozi wa Palestina ambayo imesimama dhidi ya utawala ghasibu wa Israel.

Tangu tarehe 7 Oktoba mwaka uliomalizika wa 2023, utawala wa Kizayuni wa Israel, ukisaidiwa na nchi za Magharibi hususan Marekani, umefanya mauaji makubwa katika Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan dhidi ya watu wasio na ulinzi na madhulumu wa Palestina.

Idadi ya mashahidi wa Kipalestina waliouawa kutokana na vita vya mauaji ya kimbari vya Israel dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza imefikia 26,700 na idadi ya waliojeruhiwa ni 63,740. Karibu asilimia 70 ya waliouawa au kujeruhiwa ni wanawake na watoto.