-
Kupigiwa kura ya veto maazimio yanayohusu vita vya Ghaza katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
Oct 27, 2023 03:57Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa mara nyingine tena limeshindwa kupasisha azimio Katika hali ambayo wananchi wa Ukanda wa Ghaza bado wanakabiliwa na mashambulizi ya kinyama na ya kutisha ya utawala wa Kizayuni ambapo utawala huo unazuia kufikishwa misaada ya dharura katika eneo hilo.
-
Mtazamo wa Kiongozi Muadhamu: Marekani ni mshirika katika uhalifu wa Israel
Oct 26, 2023 04:03Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amezungumzia dhulma inayokabiliwa na subira na ukakamavu wa wananchi wa Gaza dhidi ya jinai zinazoendelea kufanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel na kusema: Safari za mara kwa mara za marais wa Marekani na nchi nyingine za shari na dhalimu kama Uingereza, Ufaransa na Ujerumani huko katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu ni jaribio la kuzuia kusambaratika utawala huo ghasibu.
-
Kan'ani: Waungaji mkono wa Israel ni washirika wa jinai za utawala wa Kizayuni
Oct 25, 2023 22:56Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, kila anayeuunga mkono utawala wa Kizayuni anashiriki kikamilifu kwenye jinai za Israel na hawezi kamwe kujivua nazo.
-
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu: Utawala mbovu wa Israel unalipiza kisasi dhidi ya watu wanaodhulumiwa wa Palestina
Oct 25, 2023 11:56Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa: Utawala unaoikalia Quds kwa mabavu wa Israel uliojeruhiwa na kudhoofika, unalipiza kisasi kwa kipigo barabara cha wapiganaji wa Kipalestina katika Ukanda wa Gaza.
-
Rais Ebrahim Raisi: Jinai za Wazayuni ni sura halisi ya ubaguzi na ukoloni wa Magharibi
Oct 25, 2023 11:55Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezitaja jinai zinazofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Gaza na uungaji mkono wa nchi za Magharibi kwa jinai hizo kuwa ni sura halisi ya ubaguzi wa rangi na ukoloni wa nchi za Magharibi.
-
Kubainishwa misimamo ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuhusiana na vita vya Gaza
Oct 25, 2023 04:19Siku 19 zimepita tangu kilipoanza Kimbunga cha Al-Aqsa na vita vya utawala wa Kizayuni dhidi ya Ukanda wa Gaza. Suali muhimu la kujiuliza hapa ni je, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa na msimamo gani kuhusiana na vita hivi na imechukua hatua gani?
-
Upinzani mkali wa Marekani dhidi ya juhudi za kusitisha vita Ghaza
Oct 24, 2023 06:33Marekani ikiwa ni mshirika wa kistratijia wa utawala wa Kizayuni si tu kwamba inatoa misaada ya kila aina ya silaha na fedha kwa ajili ya kuushambuliwa Ukanda wa Ghaza, bali pia inapinga vikali usitishwaji vita katika uvamizi huo wa umwagaji damu kwa visingizio vya uongo na visivyo na msingi.
-
Jihad Islami: Misimamo ya nchi za Kiarabu na Kiislamu ni dhaifu
Oct 23, 2023 22:49Harakati ya Jihad Islami ya Palestina imetangaza kuwa misimamo dhaifu ya nchi za Kiarabu na Kiislamu inazidisha mateso na masaibu kwa watu wa Ghaza.
-
Idadi ya mashahidi wa Gaza Palestina yafikia 5087
Oct 23, 2023 08:40Wizara ya Afya ya Palestina katika Ukanda wa Gaza imetangaza kuwa, zaidi ya Wapalestina 5,000 wameuawa shahidi na wengine zaidi ya 15,000 kujeruhiwa kutokana na hujuma na mashambulio ya utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Gaza.
-
Rais wa Iran: Biden amekiri kwamba Israel ni utawala bandia
Oct 23, 2023 04:43Rais wa Jamhuri ya Kiislamu wa Iran ameyataja matamshi yaliyotolewa na Rais wa Marekani, Joe Biden, kuwa yanapinga maendeleo ya kisaisa na kijamii na demokrasia na ni dhidi ya binadamu na akasema: Matamshi ya hivi majuzi ya Rais wa Marekani ni kukiri bila hiari kwamba utawala ghasibu wa Israel ni utawala bandia.