Idadi ya mashahidi wa Gaza Palestina yafikia 5087
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i103844-idadi_ya_mashahidi_wa_gaza_palestina_yafikia_5087
Wizara ya Afya ya Palestina katika Ukanda wa Gaza imetangaza kuwa, zaidi ya Wapalestina 5,000 wameuawa shahidi na wengine zaidi ya 15,000 kujeruhiwa kutokana na hujuma na mashambulio ya utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Gaza.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 23, 2023 08:40 UTC
  • Idadi ya mashahidi wa Gaza Palestina yafikia 5087

Wizara ya Afya ya Palestina katika Ukanda wa Gaza imetangaza kuwa, zaidi ya Wapalestina 5,000 wameuawa shahidi na wengine zaidi ya 15,000 kujeruhiwa kutokana na hujuma na mashambulio ya utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Gaza.

Taarifa ya wizara hiyo imeeleza kuwa, Wapalestina 5087 wameuawa shahidi hadi sasa tangu jeshi la utawala haramu wa Israel lili[poanza kutekeleza mashambulio ya anga dhidi ya ukanda wa Gaza.

Kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Afya ya Palestina ni kwamba, kkati ya waliouawa shahidi wamo watoto 2055, wanawake 1119 na wazee 217 huku idadi ya majeruhi ikifikia 15,273.

Takwimu hizo zinatolewa katika hali ambayo, Kanali ya televisheni ya al-Mayadeen imetangaza kuwa, mashambulio ya anga ya jeshi la utawala wa Kizayuni dhidi ya Ukanda wa Gaza yanaendelea ambapo katika kipindi cha saa 24 zilizopita zaidi ya Wapalestina 500 wameuawa shahidi.

 

Tangu kuanza kwa operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa siku 16 zilizopita sawa na Oktoba 7, kushambuliwa maeneo ya makazi na umma kwa upande mmoja na kukatwa maji, umeme na uhaba mkubwa wa chakula na dawa kwa upande mwingine, kumewafanya wakazi wa Ukanda wa Ghaza kukabiliwa na hali ngumu sana na kupelekea taasisi za haki za binadamu kutangaza hali ya kibinadamu katika eneo hilo kuwa mbaya na ya kutisha.

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yakiwemo Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa, Mfuko wa Idadi ya Watu wa Umoja wa Mataifa, UNICEF, Mpango wa Chakula Duniani na Shirika la Afya Duniani yamesema katika taarifa ya pamoja kwamba: "Tunatoa wito wa kusitishwa mapigano, pamoja na kufikishwa haraka misaada ya kibinadamu huko Ghaza, ili wanaoshughulikia misaada ya kibinadamu waweze kutoa huduma kwa wananchi wanaohitaji msaada, kuokoa maisha na kuwazuia kuendelea kupata mateso zaidi."