-
Kushtadi mizozo kati ya Uturuki na Ugiriki
Mar 15, 2020 23:04Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki imemwita balozi wa Ugiriki mjini Ankara na kumkabidhi malalamiko yake kufuatia ukiukaji wa haki ya kujitawala kwenye maji ya eneo hili na kadhalika kitendo cha serikali ya Athens cha kuweka vikosi vyake katika mipaka ya nchi mbili.
-
Uturuki yasisitiza tena itaendelea kuwepo kijeshi Syria na wala haifikirii kuwaondoa askari wake Idlib
Mar 12, 2020 11:56Waziri wa Ulinzi wa Uturuki amesisitiza kwa mara nyingine kuwa nchi hiyo itaendelea kuwepo kijeshi katika eneo la Idlib nchini Syria.
-
Uturuki yakiri kuongezeka hasara za kijeshi nchini Syria
Mar 08, 2020 23:29Rais Recep Tayyip Erdoğan wa Uturuki amekiri juu ya hasara za kiroho na mali za jeshi la nchi yake huko katika mkoa wa Idlib, kaskazini magharibi mwa Syria kufuatia mapigano makali kati ya askari wa nchi mbili.
-
Bashar Asad: Syria itaanza opesheni dhidi ya wavamizi wa Kimarekani karibuni
Mar 06, 2020 04:53Rais Bashar Assad wa Syria amesema kuwa Uturuki inatekeleza maagizo ya Marekani na inafanya juu chini kuhakikisha kwamba Damascus haikomboi mkoa wa Idlib kutoka kwenye makucha ya makundi ya kigaidi.
-
Guterres apongeza makubaliano ya Russia-Uturuki kuhusiana na mgogoro wa Syria
Mar 06, 2020 04:39Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amepongeza makubaliano yaliyofikiwa baina ya Russia na Uturuki kuhusiana na usiitishaji vita katika mkoa wa Idlib nchini Syria.
-
Wahajiri kutoka Syria, kisingizio kinachotumiwa na Rais Erdoğan wa Uturuki kuushinikiza Umoja wa Ulaya
Mar 05, 2020 03:15Rais Recep Tayyip Erdoğan wa Uturuki amelikataa pendekezo la Umoja wa Ulaya kuhusu kadhia ya wahajiri na kusema: Hakuna mtu yeyote mwenye haki na ustahiki wa kuichezea ghururi ya Uturuki. Erdoğan ameyasema hayo mjini Ankara katika mkutano na waandishi wa habari aliofanya pamoja na Waziri Mkuu wa Bulgaria, Boyko Borisov.
-
Askari wa Uturuki wakimbia kwa makundi katika viunga vya Idlib, Syria + Video
Mar 04, 2020 09:54Kufuatia mashambulizi makali ya anga na mizinga ya jeshi la Syria dhidi ya maeneo ya jeshi la Uturuki katika viunga vya mkoa wa Idlib, askari wa Uturuki wameonekana wakikimbia kwa makundi katika maeneo hayo.
-
Malalamiko ya Ujerumani kwa hatua ya Uturuki ya kuzishinikiza nchi za Ulaya kupitia wakimbizi
Mar 04, 2020 04:42Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ameitaja hatua ya Uturuki ya kutumia kadhia ya wakimbizi kuishinikiza Ulaya kuwa jambo lisilokubalika kufuatia nchi hiyo kufungua mipaka yake na kupelekea kumiminika Ulaya maelfu ya wakimbizi waliokuwa wakiishi katika kambi huko Uturuki.
-
Makumi ya maelfu ya wahajiri wavuka mpaka wa Uturuki na kuingia Ulaya
Mar 03, 2020 07:58Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uturuki ametangaza kwamba hadi kufikia Jumapili usiku wahajiri wapatao laki moja walikuwa wamevuka mpaka wa nchi hiyo kuelekea Ugiriki na Bulgaria.
-
Putin: Moscow haina nia ya kuingia vitani na nchi yoyote
Mar 02, 2020 10:07Rais Vladimir Putin wa Russia ametoa radiamali yake kufuatia kushtadi mizozo kati ya nchi yake na Uturuki kuhusiana na kadhia ya Idlib, Syria na kusisitiza kwamba, Moscow haina nia ya kuingia vitani na nchi yoyote.