-
Ufaransa yamshambulia na kumtia mbaroni kiongozi wa taasisi ya Kiislamu
Oct 16, 2020 04:17Polisi ya Ufaransa imevamia nyumba ya kiongozi wa asasi moja isiyo ya kiserikali ya Waislamu wa nchi hiyo na kumtia mbaroni, katika kile kinachoonekana ni muendelezo wa hujuma dhidi ya Uislamu na Waislamu wa nchi hiyo ya Ulaya.
-
Jumuiya ya Kimataifa ya maulama wa Kiislamu yapinga matamshi ya Rais wa Ufaransa kuhusu Uislamu
Oct 03, 2020 23:17Mkuu wa Jumuiya ya Muungano wa Kimataifa wa Wanazuoni wa Kiislamu amejibu matamshi ya kihasama ya Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa kuhusu Uislamu na kusema kuwa Uislamu hauko wala hautakuwa katika mgogoro.
-
Jitihada za Macron za kuhalalisha muswada dhidi ya Uislamu nchini Ufaransa
Oct 03, 2020 23:13Hujuma na vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu barani Ulaya viliongezeka sana baada ya matukio ya Septemba 11 mwaka 2001 nchini Marekani; na mashambulizi ya kundi la kigaidi na lenye misimamo mikali la Daesh katika baadhi ya nchi za Ulaya kama Ufaransa na Uingereza yamezidisha chuki na uhasama dhidi ya Waislamu. Hivi sasa serikali ya Ufaransa ina mpango wa kupasisha sheria ya kuimarisha hujuma na vita dhidi ya Uislamu.
-
China yakadhibisha madai ya kuvunja maelfu ya misikiti ya Waislamu wa Uighurs
Sep 27, 2020 01:10Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya China imekadhibisha madai yaliyotolewa na Taasisi ya Sera za Kistratejia ya Australia (The Australian Strategic Policy Institute) ASPI ikisema kuwa makumi ya misikiti imebomolewa katika eneo la Xinjiang lililoko kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.
-
Wabunge wenye chuki wa Ufaransa wahamakishwa na hijabu bungeni
Sep 20, 2020 22:56Katika kile kinachoonekana ni muendelezo wa chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu barani Ulaya, mbunge mmoja wa chama tawala cha Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa ameongoza wabunge wenzake kutoka kwenye ukumbi wa bunge, eti kulalamikia uwepo wa mwanafunzi aliyevalia hijabu ndani ya taasisi hiyo ya taifa ya kutunga sheria.
-
Waislamu Canada wataka uchunguzi wa mauaji ya mwenzao nje ya msikiti Toronto
Sep 19, 2020 08:13Baraza la Kitaifa la Waislamu nchini Canada limetoa mwito wa kuchunguzwa mauaji ya Muislamu nje ya msikiti mmoja mjini Toronto, na kusisitiza kuwa mauaji hayo yamecochewa na chuki za kidini.
-
Amnesty International: Polisi ya India ilishirikiana na magenge ya Wahindu kuwashambulia Waislamu
Aug 30, 2020 22:03Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limesema jeshi la polisi la India lilifanya ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu kwa kushirikiana na magenge ya Wahindu wenye misimamo ya kufurutu mipaka kuwashambulia Waislamu katika mji mkuu New Delhi mapema mwaka huu.
-
Katibu Mkuu wa UN aikosoa serikali ya India kwa ubaguzi inaowafanyia Waislamu wa nchi hiyo
Aug 22, 2020 22:49Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameikosoa serikali ya India kwa ubaguzi inaowafanyia Waislamu wa nchi hiyo.
-
India yazidisha mbinyo na hatua kali za usalama eneo la Kashmir kabla ya kumbukumbu ya Agosti 5
Aug 04, 2020 08:16Serikali ya India imepiga marufuku watu kutoka nje katika eneo la Kashmir na kuzidisha hatua kali za usalama kabla ya kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu New Delhi ilipofuta mamlaka ya utawala wa ndani katika eneo hilo lenye idadi kubwa zaidi ya Waislamu.
-
Jeshi la Myanmar lajitayarisha kuwashambulia Waislamu katika jimbo la Rakhine
Jun 29, 2020 02:29Jeshi la Myanmar linajitayarisha kutekeleza oparesheni mpya dhidi ya Waislamu wa jamii ya Rohingya katika jimbo la Rakhine magharibi mwa nchi hiyo jambo ambalo limepelekea maelfu ya Waislamu kuanza kuhama eneo hilo.