-
Mkutano wa Kimataifa wataka hatua zichukuliwe kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu
Oct 02, 2023 23:15Mkutano wa kimataifa kuhusu chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia) umefanyika nchini Qatar huku mmoja wa waandalizi wake akitoa wito wa kufanyika juhudi za pamoja za kukabiliana na ongezeko la chuki dhidi ya Uislamu na athari zake "haribifu".
-
Erdogan na Anwar Ibrahim walaani kuvunjiwa heshima Qur'ani katika nchi za Ulaya
Sep 21, 2023 00:19Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, na Waziri Mkuu wa Malaysia, Anwar Ibrahim, wamelaani vikali vitendo vya kuchomwa moto nakala za Qur'ani Tukufu katika nchi za Ulaya, na hotuba zinazochochea ouvu, chuki na mashambulizi dhidi ya Uislamu na Waislamu.
-
Waislamu Marekani waishtaki FBI kwa orodha ya 'siri' ya kutotumia ndege
Sep 19, 2023 10:08Kundi la kuwatetea Waislamu nchini Marekani limeishtaki Idara ya Upelelezi, FBI, katika jaribio la kukomesha utumiaji wa orodha ya siri ambayo aghalabu inalenga Waislamu pekee kwa uchunguzi wanaposafiri kwa ndege.
-
Raisi: Umma wa Kiislamu ulioungana, ni kizuizi kwa ubeberu wa dunia
Aug 31, 2023 23:36Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema ulimwengu wa Kiislamu ambao una umoja na mshikamano ndicho kizingiti kikubwa zaidi kwa ubeberu wa dunia.
-
Hasira zatanda India baada ya mwalimu kuwataka watoto wamchape vibao mwanafunzi Muislamu
Aug 27, 2023 10:02Wimbi la hasira limeibuka nchini India baada ya kusambaa kwenye mitandao ya kijamii vidio inayomuonyesha mwalimu wa skuli moja katika jimbo la Uttar Pradesh akimdhalilisha mwanafunzi Muislamu darasani kwa kuwataka wanafunzi wenzake wamchape vibao na kutaka pia afukuzwe skulini hapo kwa sababu ya dini yake.
-
Waislamu waghadhabishwa na kuchomwa moto Qur'ani Uholanzi
Aug 19, 2023 06:58Waislamu katika kona zote za dunia wamehamakishwa na kitendo kingine cha kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu, mara hii katika mji wa The Hague nchini Uholanzi.
-
Wasiwasi wa Waislamu Ujerumani wa kuongezeka hujuma dhidi ya misikiti
Aug 17, 2023 03:54Mamilioni ya Waislamu nchini Ujerumani wana wasiwasi kuhusu kuongezeka kwa wimbi la chuki dhidi ya Uislamu na hujuma na mashambulio dhidi ya misikiti nchini humo.
-
Baada ya kushindwa kijeshi, sasa Wamagharibi wameanzisha vita vya kiitikadi dhidi ya Waislamu
Aug 05, 2023 08:06Washiriki wa Kongamano la Kielimu na Kiutafiti la "Iraq al Qur'an" wamesisitiza kuwa, baada ya kufeli na kushindwa kijeshi huko Iraq, Syria, Palestina na Lebanon, sasa madola ya kibeberu duniani yameamua kuanzisha vita vya kiitikadi na kiutamaduni dhidi ya Waislamu.
-
"Umoja ndiyo njia bora ya kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu"
Jul 09, 2023 07:23Rais wa Uturuki amesema kuna haja kwa umma wa Kiislamu kuungana na kuwa na mshikamano, ili uweze kukabiliana na vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu vilivyoshtadi katika nchi za Magharibi.
-
Iran yayaasa mataifa ya Waislamu kuungana kuzima njama za maadui
Jun 29, 2023 23:55Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Iran ametoa mwito kwa mataifa ya Kiislamu kuwa na umoja na mshikamano mkabala wa njama za maadui na lobi za Kizayuni, zenye azma ya kuibua mifarakano na ukosefu wa uthabiti katika nchi hizo.