May 21, 2023 06:34 UTC
  • Waislamu Canada walalamikia marufuku ya kusali iliyowekwa katika skuli za serikali

Waislamu nchini Canada wamelalamikia marufuku ya kusali iliyowekwa katika skuli za serikali kwenye jimbo la Quebec.

Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB limeripoti kuwa, kwa mujibu wa amri ya Waziri wa Elimu wa jimbo la Quebec nchini Canada, ni marufuku kwa vijana wa Kiislamu kutekeleza faradhi yao ya Sala katika skuli za serikali za jimbo hilo.
Waislamu wa Canada wamewasilisha malalamiko yao dhidi ya uamuzi huo na kusisitiza kwamba kupiga marufuku watu kusali katika skuli za serikali za Quebec kunapingana na Katiba ya nchi hiyo.
Jumuiya za Kiislamu nchini Canada zimeitaka mahakama itangaze kwamba uamuzi uliochukuliwa na maafisa wa jimbo la Quebec umekiuka katiba ya nchi.
Taasisi sita, ikiwa ni pamoja na Jumuiya ya Kiislamu ya Canada na Taasisi ya Waislamu wa Canada, pamoja na asasi zingine nne za jimbo hilo, zimewasilisha kesi ya kutaka Mahakama ya Juu ya Quebec itangaze kuwa amri iliyotangazwa na jimbo hilo haitekelezeki au iifute.
Asasi hizo zimesisitiza kuwa agizo hilo ni la kibaguzi na linakiuka Mkataba wa Haki na Uhuru wa Canada.
Amri hiyo wa Waziri wa Elimu wa Quebec ya kupiga marufuku watu kusali maskulini ilitangazwa Aprili 19, baada ya kupokea ripoti kwamba maafisa wa skuli zisizopungua mbili nchini Canada wanawaruhusu wanafunzi kukusanyika katika uwanja wa skuli kwa ajili ya kusali.../
 
 

Tags